Pambazuko FM Radio

Matarajio ya wanajukwaa ni kutatua changamoto za Kilimo na masoko ya mazao

19 July 2024, 8:52 pm

Jukwaa la mnyororo wa thamani wa chakula halmashauri ya mji wa Ifakara, mkoani Morogoro limechagua viongozi rasmi Julai 18, 2024 baada ya kukamilika kwa usajili wa jukwaa hilo pamoja na katiba, ambapo viongozi hao watahudumu kwa miaka mitatu Julai 2024 – Julai 2027.

Wanajukwaa baada ya kumaliza uchaguzi – Picha na: Isidory Mtunda

Na: Isidory Mtunda

Uongozi wa jukwaa la mnyororo wa thamani wa chakula, halmashauri ya mji wa Ifakara mkoani Morogoro umepania kutatua changamoto za kilimo kwa wanachma kwa kutoa mafunzo.

Hayo yamesema na mwenyekiti mteule wa jukwaa hilo mzee Mays Mkweme alipohojiwa na Pambazuko fm kujua mikakati yao baada ya uchaguzi wa viongozi wa jukwaa hilo.

Mzee Mkwembe – Mwenyekiti wa Jukwaa – Picha na Isidory Mtunda

Sauti ya mwenyekiti – Mays Mkweme

Kwa upande wao wajumbe wa jukwaa hilo, akiwemo Winifrida Pesa, Lewisi Yazidi na Hadija Furaha Muhumbira wamesema ili kulima kilimo chenye tija wanahitaji mafunzo juu ya kilimo bora na uwezeshwaji wa Pembejeo za kilimo.

wajumbe wa jukwaa

Naye afisa miradi wa shirika la Helvetas, bwana Hassan Jaha amesema; wao kama wadau watawajengea uwezo vikundi viweze kuzalisha chakula bora pamoja na kutoa elimu ya ujasiriamali ili kuongeza kipato katika maisha yao ya kila siku.

sauti ya bwana Hassan – afisa mradi wa shirika la Helvetas

Jukwaa la mnyororo wa thamani wa chakula, halmashauri ya mji wa Ifakara, mkoani Morogoro  limefanya uchaguzi wa viongozi watakaodumu kwa miaka mitatu, ambao ni; MAYS MKWEME – Mwenye kiti, DIANA MBUBA- Makamu mwenyekiti, CHRISTIAN KOMBANIA- katibu, ISSA MNANDI- Katibu msaidizi na FELIX CHIGWANDA- Mtunza hazina.