DC Kilombero apiga marufuku kuingiza mifugo ndani ya misitu ya asili Ifakara
11 July 2024, 2:52 pm
Na Katalina Liombechi
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya ameagiza wale wote wanaoingiza mifugo kwenye misitu ya asili ya Ibiki na Mbasa iliyopo kijiji cha Sululu kata ya Signal kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Wakili Kyoba ametoa agizo hilo wakati akitoa hotuba yake kwenye maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo Halmashauri ya Mji wa Ifakara yamefanyika katika kijiji cha Sululu kata ya Signali ambapo ameitaka halmashauri hiyo na wadau kuhakikisha misitu ya asili Ibiki na Mbasa kutunzwa kwa hali na mali.
Hata hivyo kwa mujibu wa wataalam wa mazingira athari za mifugo ndani ya misitu ya asili hupunguza bioanuwai, mmomonyoko wa udongo, uchafuzi wa maji, pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kipindi kuhusu maelekezo ya DC kuzuia mifugo ndani ya misitu ya asili Ibiki na Mbasa.