Bonde la Kilombero kurejeshewa mazingira ya asili, uchumi
24 May 2024, 1:15 pm
Na Katalina Liombechi
Mtandao wa Vinara wa Uhifadhi ni kama chachu ya kuamsha wadau kuwa wazalendo na Kuziishi njia za kuendeleza uhifadhi kwa kufuata njia za kurejesha asili sambamba na kuwezesha shughuli za kiuchumi rafiki kwa mazingira.
Imeelezwa kuwa Mtandao wa Vinara wa Uhifadhi wa Mazingira Katika Bonde la Kilombero utaleta matokeo chanya ya shughuli za uhifadhi wa mazingira na kufanya uchumi endelevu.
Hayo ni kwa mujibu wa Fadhili Njilimba kutoka IUCN akizungumza na Pambazuko FM mara baada ya warsha ya siku mbili ya wadau wa mazingira kutoka ndani na nje ya wilaya ya Kilombero na kufanyika katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro ikiwa ni kikao kilicholenga kuunda Mtandao wa Vinara wa Uhifadhi kama chachu ya kuamsha wadau kuwa Wazalendo na Kuziishi njia za kuendeleza Uhifadhi sambamba na kuwezesha shughuli za kiuchumi rafiki kwa mazingira na zenye Tija.
Baadhi ya Wadau walioshiriki Warsha hiyo akiwemo Mebo Kanyabua Kutoka Kampuni ya Sukari Kilombero,Saleh Shebe Afisa Usimamizi wa Mazingira kutoka Wilaya ya Kilosa na Irene Mushi kutoka TCRS Mkoa wa Morogoro wameshukuru kwa Warsha hiyo ambayo imewajengea uwezo wa Kushirikiana na kuonesha uzalendo katika uhifadhi wa Mazingira huku Uchumi wa Watu Ukiimarika.
Picha ya Mebo Kanyabua Mdau Kutoka Kampuni ya Sukari Kilombero(Picha na Katalina Liombechi)
Kikao hicho kilichofanyika Mei 16 na 17,2024 katika Ukumbi wa TTCIH Ifakara kimeitwa na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (IUCN)na Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori Afrika (AWF) ambao kwa Pamoja wanatekeleza Mradi wa Miaka Mitatu wa SUSTAIN-ECO unaolenga kurejesha Mifumo Ikolojia katika Wilaya ya Kilosa,Halmashauri ya Mlimba na Mji wa Ifakara ni Mradi unaofadhiliwa na Serikali ya SWEDEN.