Pambazuko FM Radio

Waandishi wa habari mjitofautishe na watoa Habari

1 May 2024, 7:30 pm

Mkufunzi na Mhariri wa Mtandao wa redio za Kijamii{TADIO} Hilali Alexander Ruhundwa katikati akiwa na waandishi wa Habari wa Redio Pambazuko{Picha na Maurus Kaziyareli}

Waandishi wa Habari wa Redio Pambazuko wamepigwa msasa wa mafunzo ya kuandika habari kwa kufuata maadili na misingi ya Habari.

Na Katalina Liombechi

Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,na Uchaguzi Mkuu 2025 Waandishi wa Habari wametakiwa kujitofautisha na Watoa Habari.

Mhariri kutoka RADIO TADIO Hilali Alexander Ruhundwa ameyasema hayo Baada ya Kutoa Mafunzo ya namna ya Kuandika Habari Mitandaoni na kuwakumbusha waandishi wa Habari wa Radio Pambazuko Fm kuacha kuandika habari kinyume na Maadii ya Uandishi wa Habari ili kuzuia Taharuki na Migogoro kwa Jamii.

Mkufunzi na Mhariri wa Mtandao wa redio za Kijamii{TADIO} Hilali Alexander Ruhundwa akiwawakumbusha waandishi wa Habari kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025{Picha na Keneth Ngamoga}
Sauti ya Hilali Alexander Ruhundwa Mkufunzi na Mhariri wa Mtandao wa redio za Kijamii{TADIO}