Wakazi uwanja wa taifa A mjiini Ifakara wakosa huduma za maji na choo kutokana na mafuriko.
22 April 2024, 6:49 pm
Na: Katalina Liombechi
Mafuriko yamekuwa chanzo cha kukosa huduma muhimu za kibinadamu, kama vile; maji ya kunywa, vyoo, malazi na hata chakula. Hali hiyo pia imesimamisha baadhi ya shughuli za kila siku kwa kaya zilizokumbwa na mafuriko, hivyo njaa, magonjwa ya matumbo, kuhara, typhoid kipinndupindu na hatimaye kifo.
Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Uwanja wa Taifa A kata ya Viwanyasitini Katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoa wa Morogoro wameelezea wasiwasi wao kukumbwa na Magonjwa ya Mlipuko kufuatia vyoo kujaa maji kutokana na Maji kufurika Kwenye Makazi yao.
Hayo yamesemwa na wakazi wa mtaa huo akiwemo;Tatu Abdala Ndota na Baraka Elia ambapo wamesema imekuwa vigumu kupata huduma ya choo katika Makazi yao kwa sasa kutokana na mafuriko ya maji katika maeneo yao.
sauti ya Tatu Ndota na Baraka Elia
Kufuatia hali ya Mafuriko katika Maeneo mbalimbali ya Mji wa Ifakara, Afisa afya Halmashauri hiyo Jafari Ngogomela amewataka Wakazi waliofikwa na mafuriko kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko yanayoweza kujitokeza.
Ngogomela ameyasema hayo wakati akipita kutoa elimu ya tahadhari ya Athari za Kiafya na kuwaomba Wananchi wa Kata ya Viwanjasitini na Maeneo mengine Kama Mbasa na Katindiuka kuzingatia kanuni za afya kwani maji hayo ni hatari kutokana na Kupita kwenye maeneo ya vyoo.
Amesema wao kama Halmashauri tayari wamechukua Tahadhari kadhaa ikiwa ni pamoja na Kutibu Maji katika visima vikubwa 20 Vya Kijamii kwa Kushirikiana na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Ifakara IFAUWASA.
sauti ya afisa afya – Jafari Ngogomela
Naye Diwani wa Kata ya Viwanjasitini Mh Erick Kulita amewaomba wananchi wake kutoka Maeneo hayo na Kwenda kupata Huduma kama maji na ya matumizi ya vyoo katika maeneo mengine.
sauti ya Diwani – Eric Kulita