Waathirika wa mafuriko Kilombero wapokea mssaada wa chakula tani 6
17 April 2024, 11:31 pm
mifuko ya chakula – Picha na; Katalina Liombechi
Kufuatia Adha ya Mafuriko katika Maeneo mbalimbali Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro,Kampuni ya Sukari Kilombero imekabidhi tani 6 za Vyakula zenye thamani zaidi ya Sh Mil 14 kusaidia Waathirika wa Mafuriko.
Na: Katalina Liombechi
Msaada huo wa Kibinadamu umekabidhiwa na Kampuni hiyo Kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya ambapo kwa Mujibu wa Meneja Mahusiano wa Kilombero Sugar Company Victor Bemelwa ametaja vyakula hivyo kuwa ni pamoja na Unga tani 2, mchele tani 2 na maharage tani 2 na kwamba utazifikia kaya 500 za Waathirika wa mafuriko katika Halmashauri ya Mlimba na Mji wa Ifakara.
sauti ya Meneja mahusiano
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya akipokea msaada huo ameelezea shukrani zake za dhati kwa Kampuni ya Kilombero Sukari kwa msaada huo ambapo amesema atahakikisha unawafikia walengwa.
Mkuu wa wilaya akiongea baada ya kupokea msaada (mwenye koti) – Picha na; Katalina Liombechi
sauti ya DC Kyobya
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Wilaya ya Kilombero ilikumbwa na mafuriko katika maeneo mbalimbali ambapo baadhi ya maeneo yaliyoathirika zaidi ni pamoja na Kata za Masagati na Utengule halmashauri ya Mlimba huku Katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara mafurika hayo yakiathiri kata za Viwanja sitini, Mbasa, Lipangalala, Mlabani, Lumemo na Kusababisha Kifo cha Kijana mmoja, Shafii Kambeyu mkazi wa Kata ya Katindiuka