Pambazuko FM Radio

Waathirika wa mafuriko Ifakara wapata msaada

10 April 2024, 11:37 pm

Exif_JPEG_420

Picha ya waathiriika wakiwa kwenye moja ya kambi – Picha na Katalina Liombechi

Na Katalina Liombechi

Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mh Aboubakar Asenga Ametoa Msaada wa vyakula kwa Waathirika wa Mafuriko 135 walioweka kambi katika Shule ya Msingi Kiyongwile Kata ya Lipangalala na Lumemo Waathirika 18 walioweka Kambi katika Shule ya Sekondari Mahutanga.

Msaada huo ameutoa alipotembelea Kambi hizo ambapo ametoa msaada wa  vyakula vikiwemo; Unga,Sukari na Mafuta ya kula huku akiwaomba wananchi hao kuwa wavumilivu kwani changamoto ya Mafuriko tayari ameifikisha Bungeni.

Exif_JPEG_420

Mbunge akigawa msaada kwa baadhi ya wananchi – amevaa T-shirt ya Kijani – Picha na Katalina Liombechi

Sauti ya Mbunge

Diwani wa Kata ya Lumemo Mh.Frank Ngao na Mwananchi wa Lipangalala Bi Malisela Makwinya wamemshukuru Mbunge kwa Msaada huo ambao wamesema unakwenda kupunguza ukali wa maisha kwa wathirika wa Mafuriko hasa kipindi hiki kigumu wanachopitia.

Sauti ya Diwani na mwananchi

Utakumbuka kuwa hivi Karibuni Wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara walikumbwa na Mafuriko ambapo maeneo yaliyoathirika zaidi ni pamoja na kata za; Viwanjasitini,Mbasa Katindiuka, Lumemo Lipangalala na kitongoji cha  Mbalaji kata ya Signali.