Wakazi wa Mlimba wapokea huduma za kibingwa za afya kwa furaha
15 October 2023, 10:11 am
Baadhi ya wagonjwa wakisubiri huduma za kibingwa -Picha na Isidory Matandula
Madaktari bingwa wa mfumo wa mkojo na ENT (Ear, Norse and Throat) kutoka hospitali ya rufaa ya Mtakatifu Fransisko, Ifakara, wiki hii wametoa huduma za kibingwa katika Kituo cha Afya Mlimba, Halmashauri ya Mlimba, wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro.
Na Isidory Matandula
Wakazi wa Mlimba halmashauri ya Mlimba wamenufaika na huduma za kibingwa kotuku kwa madaktari bingwa wa Hospitali ya rufaa ya Mtakatifu Fransisko ya mjini Ifakara.
Mzee Bernard Mapunda na Blandina Cletus ni miongoni mwa wananchi walionufaika na hudumahiyo, ambapo mzee mapunda amezibuliwa masikio na mtoto Ronclif mwenye umri wa wiki mbili ameongezewa njia ya mkojo.
Mzee Mapunda – Picha na Isidory Matandula
Nta za masikioni kutoka kwa mzee Mapunda – Picha – Isidory Matandula
Sauti za wananchi waliopata huduma za afya za kibingwa
Nao madaktari bingwa Elias Marandu na Anthoni Magoda, wamesema mwitikio umekuwa mzuri, ambapo wagonjwa walioonwa nao wamefurahi na wamenufaika na kliniki hiyo Mkoba na wameahidi kuwa itakuwa endelevu.
Dr. Marandu na mzee Mapunda – Picha na Isidory Matandula
sauti za madaktari bingwa – Magoda na Marandu
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa kituo hicho, Herman Mnema Mganga, ameomba huduma hiyo ifanyike walau mara moja kwa mwezi au kila baada ya miezi mitatu.
Mganga mfawidhi kituo cha afya Mlimba – Picha na Isidory Matandula
Sauti ya mganga Mfawidhi