Waganga tiba asili, mbadala waagizwa kuzingatia maadili
29 June 2023, 10:45 pm
Waganga wa tiba asili na tiba mbadala mji wa Ifakara – Picha na; Isidory Mtunda
Waganga wa tiba asili na tiba mbadala halmashauri ya mji wa Ifakara, wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wameagizwa kufanya huduma ya kuponya wagonjwa na kuachana na masuala ya ramli na kusafisha nyota.
Na; Isidory Mtunda
Waganga wa tiba asili na tiba mbadala wametakiwa kuacha utapeli na upigaji ramli, vitendo ambavyo baadhi yao wamekuwa wakijihusisha navyo.
Rai hiyo imetolewa na mratibu wa waganga wa tiba asili na tiba mbadala halmashauri ya mji wa Ifakara Dkt. Fadhili Jeremia Fabian, katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji kata ya Kibaoni, wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro kwa lengo la kupokea kero zao.
Mratibu wa tiba asili na tiba mbadala Dkt. Fabian – Picha na Isidory Mtunda
Dkt. Fabian amewaagiza waganga hao kuwa huduma zao zilenge kuponyesha wagonjwa na si kufanya mambo ya pete, kusafisha nyota na upigaji ramli, mambo ambayo baadhi yao wamekuwa wakijinadi kwayo.
sauti ya Dkt. Fabian
Naye mwenyekiti wa umoja wa waganga wa tiba asili na tiba mbadala Tabibu Joseph Nyakigali, amewataka waganga wenzake wawe na upendo na kufanya kazi kwa ushirikiano na amewataka kujenga urafiki na wenye mafanikio.
Sauti ya tabibu Nyakigali
Kwa upande wao baadhi ya waganga hao Fatuma Ahamad na Ibrahimu Lihundi wameiambia Pambazuko fm kuwa waganga hao hawapendani na baadhi yao wamekuwa wakitoa kejeli kwa wenzao kuwa hawana dawa, hasa waganga wanaotoka nje ya halmashauri ya mji wa Ifakara.
mganga wa tiba asili Fatuma Ahamed – picha na; Isidory Mtunda
sauti za waganga wa tiba asili