Pambazuko FM Radio

Watafiti waja na drones kutokomeza mazalia ya mbu

21 February 2023, 3:07 pm

Na Rifat Jumanne

Watafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa Afya Ifakara wameanzisha program maalum ya kutumia ndege zisizo na rubani {Drones} ambazo zitakuwa na uwezo wa kuzunguka na kunyunyizia dawa ili kudhibiti ugonjwa wa malaria katika Mji wa Ifakara.

Najat Kahamba ni mtafiti anayejihusisha na uelewa wa tabia na mazingira ya mbu{Picha na Rifat Jumanne}

Hayo yamebainishwa katika mkutano maalumu ulioandaliwa na wanasayansi ndani ya idara ya afya ya mazingira na sayansi ya ikolojia(EHES) ambapo uliwakutanisha na viongozi wa wilaya,kata na vijiji kutoka ndani ya bonde la kilombero mjini Ifakara ili kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu kazi zinazofanywa na taasisi hiyo.

Mbu aina ya anopheles phonesta anasadikika kueneza kwa kiasi kikubwa maambukizo ya malaria katika mji wa ifakara

Najat Kahamba ni mtafiti anayejihusisha na uelewa wa tabia na mazingira ya mbu anayeitwa anopheles phonesta ambaye anasadikika kueneza kwa kiasi kikubwa maambukizo ya malaria katika mji wa ifakara yeye amesema ili kupamba na mbu aina hiyo watafiti wanatakiwa  kujua uwepo wa mbu huyo anapatikana wapi,anaishije na wanzaliana wapi  pamoja na kujua vitu vinavyosababisha kuendelea kuzaliana kwake.

Amesmea hapo awali tafiti zilizokuwa zikifanywa dhidi ya mbu huyo watafiti walikuwa wakitumia  picha za satilait ambazo kwa kiwango kikubwa ilikuwa ngumu kutambua  baadhi ya picha kutokana na udogo wake hivyo kushindwa kutambua baadhi ya tabia za anopheles phonestansi huyo.

Sauti ya mtafiti anayejihsisha na uelewa wa tabia ya Mbu Najat Kahamba akielezea drone

Kwa upande wake Faraja Billah ambaye ni mratibu wa masuala ya utafiti kwa jamii kwenye kituo cha utafiti wa afya ifakara amesema lengo kuu la mkutano huo ni kufahamiana na viongozi wanaopatikana katika maeneo ya kiutafiti ,kupeleka uelewa wa kiutafiti kwa jamii na kueleza shughuli wanazofanya katika kituo hicho.

Mratibu wa masuala ya utafiti kwa jamii kwenye kituo cha utafiti wa afya ifakara Faraja Billah

Baadhi ya viongozi wa kata,vijiji na wanajamii wamewashukuru wanasayansi hao kwa kuona umuhiumu wa kuishirikisha jamii katika kazi zao mbalimbali na hata hivyo hawakusita kuwapongeza kwa kuileta teknolijia mpya kutumia drones katika kuua mazalia ya mbu ili kutokomeza ugonjwawa malaria katika maeneo yao kwani ugonjwa huo umekuwa ukipoteza maisha ya watu wengi na kuchelewesha maendeleo katika jamii.

Viongozi wa vijiji na kata wakifuatilia mkutano{Picha kutoka maktaba}
Sauti ya Baadhi ya viongozi wa kata,vijiji na wanajamii wakiwashukuru wanasayansi hao kwa kuona umuhiumu wa kuishirikisha jamii katika kazi zao