Wavuvi Funga Waiangukia Serikali ya Kijiji,Waomba Waachwe
1 July 2021, 6:11 am
Wavuvi katika Kambi ya Funga iliyopo katika kijiji cha Kivukoni Kata ya Minepa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga wameuomba Uongozi wa Kijiji hicho kuwaacha waendelee kubaki katika Kambi hiyo kufanya shughuli za Uvuvi huku wakieleza kuwa wako Tayari kufuata taratibu watakazopewa na Kijiji hicho.
Akizungumza kwa Niaba ya Wavuvi wa kambi hiyo Mbele ya Diwani wa Kata hiyo Malugu Manosu na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wa Kata hiyo Costantine Mbeya,.Mariam Abdalah amesema wao wamekuwa wakifanya shughuli hiyo Muda Mrefu katika kambi hiyo na kuwasaidia kuendesha Maisha yao.
Aidha Wamesema Ombi hilo likikubaliwa wako tayari kufanya usajiri wa kambi hiyo na kufuata maelekezo yoyote yatakayotolewa na Serikali ya Kijiji hicho.
Pambazuko fm Ililazimika kumtafuta Mwenyekiti wa Kijiji hicho Shaneli Masasi kuzungumzia suala hilo ambapo ameeleza kuwa Tayari walishakubalina kuwa wataondoka katika kambi hiyo kwa Muda Uliopangwa.
Aidha amesema kambi hiyo siyo rasmi na iko katika eneo la Hifadhi ya ILUMA huku akidai kuwa baadhi ya Wavuvi hao wamekuwa wakifanya uvuvi Haramu.