Boma Hai FM
Boma Hai FM
20 March 2026, 4:20 am

Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi katika wilaya ya Hai kutotoka site bila sababu ya msingi mpaka miradi itakapokamilika.
Na Henry Keto, Hai-Kilimanjaro
Mbunge wa jimbo la Hai Mhe. Saashisha Elinikyo Mafuwe amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi mbalimbali ndani ya Jimbo la Hai kufanya kazi usiku na mchana bila kusuasua na kutotoka site bila sababu za msingi mpaka miradi hiyo itakapokamilika.
Wito huo umetolewa Machi 19,2026 wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika wilaya ya Hai, miradi iliyotembelewa ni Barabara ya makoa – mferejini inayojengwa kwa urefu wa kilometer 7 ambapo awali mkandarasi alionesha kushindwa kutokana na usanifu wa awali na sasa amerejea kuendelea na kazi, Ujenzi wa daraja la Saashisha linalounganisha kikavu chini na Mkalama katika kata ya Mnadani na kata ya Weruweru.
Mfuwe amemtaka mkandarasi anayejenga barabara ya makoa mferejini kutotoka site mpaka atakapokamilisha mradi kwasababu mwanzo barabara ilisimama kwa kipindi cha muda kutokana na hali ya mradi hivyo ahakikishe aondoki site mpaka atakapokamilisha ujenzi wa mradi huo wa barabara, vilevile amemtaka kutosuasua kwa mradi kwani pesa yote ameshalipwa.

Pia, amewaomba wananchi kulinda miradi ya barabara kwa uchungu mkubwa kwasababu miradi hiyo inatumia fedha nyingi kujengwa, aidha amewataka kutoacha maji ya mfereji kupita kwenye barabara bali kuyaekekeza kwenye mitaro iliyopo pembezoni mwa barabara kwakushirikiana kwa karibu na wenyeviti pamoja na madiwani.
Nae mkandarasi Frenk Mafie amethibitisha kupokea fedha zote za mradi na kuahidi kutotoka site mpaka mradi utakapo kamilika, vile vile amesema wameshaweka mikakati mizuri yakuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na tayari vifaa vipi site na kazi imeanza.
