Boma Hai FM
Boma Hai FM
3 December 2025, 12:33 pm
“Mikopo mnayopewa wekezeni kwenye shughuli za uzalishaji” Dc Bomboko

Halmashauri ya wilaya ya Hai imetoa mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani yasiyo na riba yenye jumla ya shilingi millioni 247.1 kwa vikundi 29 vilivyokidhi vigezo vyakupata mikopo hiyo
Na Henry Keto, Hai-kilimanjaro
Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe Hassan Bomboko amewataka Wananchi kuwekeza kwenye shughuli halali zenye kuleta kipato kwa Wananchi,pamoja na kutumia fursa zilizopo kwenye jamii ya wilaya ya Hai
Hayo yamesemwa Leo December 02,2025 wakati wa ugawaji wa hundi za Mikopo ya Serikali ya asilimia 10 isiyo na riba inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri yenye jumla ya Shilingi Million 247.1.
Aidha Bomboko amewataka vijana kuacha kufanya shughuli zisizo halali Bali wafanya taratibu wapate Mikopo ili wajikwamue kwenye wimbi la umasikini, vilevile amewataka kuacha kuwekeza kwenye kubeti

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ametoa wito Kwa Wananchi kuepuka maneno yasiyorasmi yanayoposha Umma kuhusu Mikopo hiyo, amesema kwa kipindi cha awamu ya sita Halmashauri ya wilaya ya Hai imetoa Mikopo ya pikipiki 35 kwa vikundi 9 vya Vijana, Bajaj 4 kwa vikundi viwili na Guta 5 kwenye vikundi 3
Nae kiongozi wa mafunzo kwa wanufaika wa Mikopo hiyo Ibrahim Hamisi Mkindi ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kutoa fedha hizo kwaajili ya watanzania, vilevile ametoa wito Kwa wanufaika kufanya biashara na kurejesha kwa wakati.
Wanufaika wa Mikopo hiyo wameeleza namna gani wanaenda kuitumia Mikopo hiyo kujinufaisha na kujikwamua kiuchumi, lakini pia wameeleza Mikopo hiyo imetolewa kwenye vikundi vilivyokidhi vigezo.
Sauti za wanufaika wa mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri