Boma Hai FM

Wakandarasi Wilaya ya Hai Wametakiwa kukamilisha miradi kwa wakati

26 November 2025, 3:12 pm

Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai (Kushoto) Ndugu Dionis Myinga akiwa na Mkandarasi wa Paric Limited (Kulia) Paul Abel baada yakusaini mkataba wa ujenzi wa jengo la Halmashauri.(Picha na Henry Keto)

Halmashauri ya wilaya ya Hai imesaini mkataba wa ujenzi wa jengo jipya na lakisasa la ofisi za halmashauri lenye thamani ya Shilingi Bilioni 4.39 unaojengwa kwa muda wa miaka miwili mpaka Novemba 25,2027 unaotekelezwa na kampuni ya Paric limited.

Na Henry Keto, Hai-Kilimanjaro

Wakandarasi wanaotekeleza miradi mbalimbali katika wilaya ya Hai wameaswa kumaliza miradi kulinga na muda uliopangwa kwenye mikataba yao, Pamoja na kutekeleza miradi hiyo kwa ubora unaotakiwa kwa kulingana na thamani ya fedha.
Wito huo umetolewa na mkuu wa wilay ya Hai mhe. Hassan Bomboko wakati akishuhudia zoezi la utiaji Saini wa mkataba wa ujenzi wa jengo jipya la kisasa la ofisi za halmashauri ya wilaya ya Hai unaogharimu kiasi cha shilingi 4.39 Billioni

Sauti ya Mkuu wa wilaya akizungumza kuhusu baada yakushuhudia zoezi la musaini mkataba wa jengo la ofisi za halmashauri.

Mkurugenzi Mtendaj wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Ndugu Dioni Myinga ameishukuru serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa jengo jipya na lakisasa la Ofisi za Halmashauri yenye Idara 21.Myinga amewashukuru viongozi mbalimbali walikuwa mstari wa mbele katika kupanga nakufikisha ajenda za ujenzi wa jengo hilo lenye thamani ya Shilingi Billion 4.39.

Pichani ni Viongozi wa wilaya ya Hai wakishuhudia zoezi la Utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa jengo la ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Hai(Picha na Henry Keto)

Nae Katibu Tawala wa wilaya ya Hai Ndugu Sospeter Magonera ametoa angalizo kwa mkandarasi kusaini na Kuondoka Bali ujenzi uanze haraka iwezekanavyo kulingana na mkataba wa ujenzi wa jengo hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Takukuru wilaya ya Hai Ndugu Josiah Gunda amemtaka mkandarasi kuzingatia matumizi sahihi ya Fedha katika utekelezaji wa miradi huu wenye gharama kubwa,ikiwa ni pamoja na kuzingatia muwa wakimaliza mradi, material test pamoja na ubora wa jengo kulingana na thamani ya Fedha.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai, Sauti ya katibu tawala wa wilaya ya Hai Ndugu sospeter Magonera na Mkuu wa takukuru wilaya ya Hai

Nae mhandisi wa wilaya Matandiko Anold amesema kuwa muda wa ujenzi wa mradi huo ni muda wa miaka miwili ambalo ni jengo la nghorofa moja lenye uwezo wa kuwa na Idara zote 21 za halmashauri ya Hai

Sauti ya Mhandisi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Anold Matandiko akizungumza baada yakukabidhi mradi kwa mkandarasi wa Paric limited.
Pichani ni Wakuu wa idara 21 za Halmashauri ya wilaya ya Hai wakishuhudia makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi za halmashuri.(picha na Henry Keto)

Zoezi hilo limefanyika novemba 25,2025 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Hai ambapo pia Bomboko amewaasa viongozi wote kukusanya mapato ya ndani kwa weledi ili kuendeleza miradi mingine ndani ya wilaya, mradi huu mkubwa unategemewa kujengwa kwa miaka miwili kuanzia siku ya kusaini ambayo ni Novemba 25,2025 hadi Novemba 25,2027.