Boma Hai FM

DC Bomboko akagua miradi Hai, asisitiza amani

25 November 2025, 11:59 am

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Hai Hassan Bomboko (katikati)katibu tawala wilaya ya Hai Sospiter Magonera(anayezungumza)pamoja na mkandarasi wa mradi wa maji Kawaya(picha na Elizabeth Mafie)

Mkuu wa Wilaya ya Hai Hassan Bomboko akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maji na barabara wilayani Hai, amewataka wananchi kuilinda amani ili miradi hiyo ikamilike na kuleta maendeleo.

Na Elizabeth Mafie Hai-Kilimanjaro.

Wananchi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuilinda na kuitunza amani iliyopo, kwani ni msingi muhimu wa upatikanaji wa maendeleo katika jamii.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Hassani Bomboko wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya kimkakati Novemba  24,2025.

Pichani ni mkuu wa wilaya wa Hai Hassan Bomboko (Kulia)akizungumza na wananchi wanaopata huduma ya maji katika kulula cha maji kwa sadala kitongoji cha Matowo(picha na Elizabeth Mafie)

Akizungumza katika ziara hiyo, Bomboko amesema miradi inayoendelea kutekelezwa inalenga kutatua changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama, pamoja na miundombinu ya barabara ili kuboresha maisha ya wananchi.

Amesema ameridhishwa na hatua ya utekelezaji wa miradi hiyo, ikiwemo ujenzi wa tanki la maji la Kawaya na daraja la Nkwarungo lililopo Longoi, Kata ya Weruweru Miradi hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja imefikia hatua ya asilimia 50 ya utekelezaji huku akiwataka wakandarasi kuongeza kasi ili kuhakikisha kazi inakamilika kwa wakati uliopangwa.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Hai Hassan Bomboko

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Wilaya ya Hai Mhandisi Emmanuel Mwambashi, amesema ujenzi wa tanki la maji Kawaya unagharimu zaidi ya shilingi milioni 600. Ujenzi huo ulianza Februari 2024 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 30, 2026, ambapo utaanza kuhudumia zaidi ya wananchi 8,000 wa eneo hilo.

Sauti ya meneja RUWASA wilaya ya Hai Mhandisi Emmanuel Mwambishi

Naye Meneja wa TARURA Wilaya ya Hai Mhandisi Kuya Francis, amesema mradi wa ujenzi wa Daraja la Nkuarungo unagharimu zaidi ya shilingi milioni 500 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 30 mwaka huu.

Sauti ya meneja TARURA wilaya ya Hai Mhandisi Kuya Fransis

Katika hatua nyingine Bomboko alitembelea kilula cha maji kilichopo Kijiji cha Kwasadala, Kitongoji cha Matowo na kujionea namna wananchi wa eneo hilo wanavyonufaika na huduma ya maji safi na salama.

Mradi wa ujenzi wa daraja nkwarungo lililopo kata ya Weru Weru kijiji cha Longoi(picha na Elizabeth Mafie

Baadhi ya wananchi wanaotumia kilula hicho wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakisema kuwa kitongoji hicho hakijawahi kupata maji tangu uhuru. Wamesema kuwa sasa wanapata huduma ya maji safi na salama kwa wakati, hali iliyowawezesha kuendelea na shughuli za maendeleo.

Sauti za wananchi wanaotumia Kilula cha maji kwa Sadala kitongoji cha Matowo wakiishukuru serikali.