Boma Hai FM

Watumishi Hai waishukuru serikali ongezeko la mishahara

29 July 2025, 2:11 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan (Picha kwa msaada wa mtandao)

Watumishi wa umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai wameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaongezea mishahara kutokana na ahadi aliyoitoa siku ya Mei mosi 2025 mkoani Singida.

Na Henry Keto, Hai-Kilimanjaro’

Watumishi wa umma katika Wilaya ya Hai wamemshukuru kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uamuzi wake wa kuongeza mishahara ya watumishi wa umma kwa asilimia 33.1%,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (International Workers’ Day), Mei 1, 2025, Mkoani Singida, Rais Samia alisema kwamba mshahara mdogo wa watumishi uliongezeka kutoka TZS 370,000 hadi TZS 500,000 kwa mwezi hii inaonyesha kuthamini kazi ngumu mliyofanya katika kukuza uchumi, hata wakati tulipowalazimisha kuwa makini kwenye matumizi.

‎Watumishi wa wilaya ya Hai wametoa pongezi na shukrani katika mazungumzo malum na radio Boma Hai FM baada ya Raisi Dkt Samia Suluhu Hassan kuongeza mshahara kwa Watumishi wa Umma Hadi kufikia kiwango cha chini laki tano kutoka laki tatu,ambapo kila mmoja ameongezewa kutokana na mshahara wake kazini wengine kwa asilimia 33.1%

‎Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Ndg Robert Mwanga ametoa pongeza kwa mama samia na Kwa Watumishi ambao wamenufaika na ongezeko la mishahara katika idara ya maendeleo ya jamii jambo ambalo litaongeza ufanisi katika kazi za kuwatumikia wananchi, aliwahimiza watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma kama sehemu ya kutambua juhudi zinazofanywa na serikali katika kuboresha maslahi yao.

“Tuna wajibu wa kumrudishia Rais Samia kwa vitendo kwa kuwahudumia wananchi kwa uadilifu, upendo na tija zaidi sasa tunamuahidi raisi utumishi uliotukuka, sisi hatumdai mama ila mama anatudai kazi,”

Sauti ya Robert Mwanga Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii wilaya ya Hai

Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Hai ameshukuru serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na kuahidi kufanya kazi kwa weledi na kuwatumikia wananchi kwa ukaribu zaidi na pia kama mwanamke ameona adha wanazokumbana nazo wazazi katika malezi, hivyo ameahidi kuungana nae katika kila jambo.

“Kwa kweli tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita. Mama Samia ameonesha kuwa ni kiongozi anayejali maisha ya watumishi wake, Ongezeko hili limetufungua macho na mioyo,Tumepewa matumaini mapya,”

Sauti ya Hilda Gada Kiria Afisa maendeleo wilaya ya Hai

Afisa umwagiliaji na mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi mkoa wa Kilimanjaro TUGHE ndugu Msafiri msuya ametoa pongeza kwa mama samia na wafanyakazi wote walionufaika na ongezeko hilo, amewataka kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo katika nchi yetu ya Tanzania, pia kwa niaba ya chama cha wafanyakazi TUGHE ameahidi kuungana nae Kwenye kila jambo la maendeleo na kumuunga mkono October kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Kwa niaba ya watumishi wengine wa wilaya ya Hai afisa Kilimo ndugu Deogratias Sung’are na Afisa mtendaji kijiji cha Kware Ndugu Edwine Lamtey wametoa shukrani kwa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia suluhu Hassan kwa kuona umuhumu wa watumishi wa umma katika sekta mbalimbali hapa nchini kwa kuongeza mishahara na posho kwa wafanyakazi wote wa serikali ns kushidi kuendelea kuwatumikia wananchi kwa weledi mkubwa pia kuunga mkono juhudi za raisi katika kuleta maendeleo hapa nchini Tanzania.

Sauti za Afisa Kilimo wilaya ya Hai Deogratius Sung’are na Afisa mtendaji kijiji cha Kware ndugu Edwine Lamtey