Boma Hai FM
Boma Hai FM
19 July 2025, 9:01 am

Katika kuendelea kumtukuza Mungu kupitia muziki wa injili mkurugenzi wa tuzo za East Africa Gospel Music Awards apandisha tuzo hiyo kilele cha mlima Kilimanjaro.
Na Elizabeth Noel.
Moshi -Kilimanjaro
Tuzo ya Afrika Mashariki ya Muziki wa injili ( East Africa Gospel Music Awards( EAGMA )imepandishwa Katika Kilele Cha Mlima Kilimanjaro kupitia Geti la Marangu lililopo Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro .

Akizungumza kwa Njia ya simu mkurugenzi wa tuzo za East Africa Gospel Music Awards (EAGMA) Magreth Chacha amesema lengo la tuzo hiyo kupandishwa mlima Kilimanjaro ni kwaajili ya Utukufu kwa Mungu na kuuheshimisha Muziki wa injili.
Tuzo hiyo inatarajiwa Kufikishwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro na kushushwa siku ya jumamosi ya Julai 19,2025 huku mgeni rasmi katika mapokezi ya tuzo hiyo akitarajiwa kuwa Askofu Fredrick Shoo