Boma Hai FM
Boma Hai FM
1 July 2025, 8:34 pm

Mikopo ya Shilingi milioni 220 imetolewa kwenye vikundi 31 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, zaidi ya Bilioni moja milioni mia tisa sitini na nane zimetolewa wilayani hai kwa kipindi cha miaka minne.
Na Henry Keto, Hai-Kilimanjaro
Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Hassan Bomboko amevipongeza na kuvitaka Vikundi vya akina mama,vijana na watu wenye ulemvu vinavyonufaika na mikopo ya asilimia 10 ya Mapato ya ndani ya serikali isiyo na riba kutumia mikopo hiyo vizuri kuondoa umasikini na kuinua uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
Mhe. Bomboko ametoa pongezi hizo na wito siku ya Leo July 1,2025 wakati akikabidhi hundi ya Shilingi Millioni mia mbili ishirini na laki Saba kwenye Vikundi 31 ambayo ni Vikundi 6 kwa vijana, Vikundi 6 kwa watu wenye ulemavu na Vikundi 19 vya wakina mama.
Aidha ametoa takwimu za utoaji wa mikopo ndani ya wilaya ya hai kwa kipindi cha miaka minne zaidi ya Bilioni Moja millioni mia tisa sitini na nane (1,968,000,000/=), na Kwa kipindi cha mwaka mmoja imetolewa mikopo ya Shilingi Millioni mia tisa Kumi na tisa laki Saba na elfu thelathini na Saba (919,737,000/=), ambalo kuanzia 2020-2025 zaidi ya Vikundi 329 vimenufaika na mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba.
Nae Katibu Tawala wa wilaya ya Hai ndg. Sospeter Magonera amesema lengo la mikopo hii nikuondoa umasikini na kuinua uchumi, na amewaasa kuacha tabia za kutumia mikopo kwa matumizi yasiyodhamiriwa wakati wa ukaguzi kabla yakupewa mikopo hiyo, ametoa rai hasa kwa wanawake ambao huwa na tabia zakutumia mikopo kwaajili ya shughuli za ndoa na kitchen party.

Seif Charles Seifu ni kijana aliyenufaika na mikopo hiyo ameishukuru serikali kwa kupata mikopo huo,amesema utamsaidia Kuondoka na umasikini na yeye na kikundi chake watakuwa Waaminifu kurudisha mikopo hiyo kwa wakati.
Wananchi walionufaika na na mikopo hiyo wameishukuru serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania kwa kutoa mikopo itakayosaidia wanawake vijana na watu wenye ulemavu kujikimu na kuondokana na hali ya umasikini na kuinua uchumi wa familia na uchumi wa taifa