Boma Hai FM
Boma Hai FM
9 June 2025, 12:51 pm

Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Hai kimempokea mwenezi wa chama hicho CPA Amosi Makala katika ziara yake kwenye mikoa ya Kaskazini na kuzungumza na wananchi wa wilaya ya Hai.
Na Oliver Joel, Hai-Kilimanjaro
Katibu mkuu mwenezi wa CCM Taifa CPA Amosi Makalla amesema kuwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo yaliyofanywa kwa kuzingatia ilani ya chama cha mapinduzi ndio sababu kubwa iliyopelekea wananchi kuendelea kukiamini chama na kuchagua viongo zi wanaotokana na chama hicho.
Ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa wilaya ya Hai ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya
Kikazi mkoani Kilimanjaro.
Amesema kuwa miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika wilaya ya Hai kama vile elimu,maji barabara na afya inatokana na kazi kubwa inayofanywa na mheshimiwa Rais Samia Suluh Hasssan katika kuhakikisha kuwa anatatua changamoto za wananchi.
Ameongeza kuwa ushindi wa CCM uliopatikana kwa kishindo katika serikali za mitaa wilayani Hai ni deni kubwa kwa viongozoi wa CCM kuhakikisha kuwa wanakidhi haja na matakwa ya wananchi kwa ujumla.

Naye Mbunge wa jimbo la Hai Mheshimiwa Saashisha Mafuwe amemshukuru Rais Samia Suluh Hassan kwa fedha nyingi ambazo amekuwa akizitoa kwa ajili ya jimbo la Hai ambapo mpaka sasa zahanati mpya nane zimejengwa wilayani Hai ambapo nyingine zimeshakamilika huku baaadhi ujenzi wake ukiwa unaendelea,
Ziara hiyo ya katibu mkuu mwenezi Taifa Amos Makala inafanyika katika mikoa mitatu katika kanda ya kaskazini ambayo ni Arusha Manyara na Kilimanjaro.