Boma Hai FM
Boma Hai FM
4 June 2025, 4:23 pm

Katika kuelekea maadhimisho ya kilele cha wiki ya Mazingira Duniani Wilaya ya Hai imepanda miti zaidi ya elfu moja katika maeneo mbalimbali ndani ya wilaya hiyo.
Na Henry Keto
Afisa Tawala Wilaya ya Hai Marry Mnyawi amewaasa wananchi wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro kuwa na utamaduni wakupanda miti kwenye maeneo yao na kutunza mazingira kila eneo watakalokuwepo.
Mnyawi amesema hayo wakati wa upandaji miti katika kata ya KIA Kwenye kitua kipya cha Afya kinachoendelea kujengwa kwa Fedha za Mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo miti Zaidi ya 356 imepandwa kuzunguka kituo hicho.
Hatua hii inakuja ikiwa ni wiki ya mazingira Duniani ambapoa maadhimishi Kwa mkoa wa Kilimanjaro yatafanyika Wilayani Hai siku ya Alhamic June 5,2015 yenyewe kauli mbiu “Mazingira Yetu na Tanzania ijayo tuwajibike Sasa dhidi ya Matumizi ya plastiki”
Pia ametoa wito kuendelea kuitunza miti hiyo iliyopandwa alisema kupanda miti ni hatua moja na kuhakikisha inakuwa ni hatua nyingine.

Afisa mazingira Wilaya ya Hai Alfred Njigite amesema Kuelekea kilele cha Wiki ya Mazingira Duniani Miti Zaidi ya 1000 Kupandwa maeneo mbalimbali katika Wilaya ya Hai.
Siku ya Leo miti Zaidi 356 imepandwa Kata ya KIA Kwenye Kituo kipya cha Afya cha KIA kinachojengwa na Fedha za ndani za Halmashauri, maadhimisho ya wiki ya mazingira yanaenda na kauli mbiu “Mazingira Yetu na Tanzania ijayo tuwajibike Sasa dhidi ya Matumizi ya plastiki”
Kwa upande wake diwani wa Kata ya KIA Teera Kipara Molel amewashukuru Wananchi wote wa kata ya KIA kwa kujitokeza Kupanda miti katika eneo la Kituo cha Afya cha KIA ili kuweka mazingira ya kituo hicho kuwa mazuri na kuvutia lakini pia kuunga mkono zoezi la upandaji miti katika wiki ya Mazingira Duniani.

Mwenyekiti wa CCM kata ya KIA ameishukuru serikali kwa juhudi zinazoendelea kufanyiwa kuweka mzangira yawe mazuri na yakupendeza,amewapongeza pia Wananchi waliojitokeza kupanda miti kata ya kia, wananchi nao wameishukuru serikali kwa kuwapa miti ili kupanda katika maeneo yao wanayoishi