Boma Hai FM
Boma Hai FM
29 May 2025, 2:18 pm

Pichani ni bweni la shule wa wasichana Machame sekondari likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi(picha na Faraja Ulomi)
Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wananfunzi kote na nchini,hii inaadhihirika wazi kutokana na miradi mbalimbali ya ujenzi inayoendelea huko mashuleni ikiwemo shule ya wasichana Machame.
Na Faraja Ulomi. Hai -Kilimanjaro
Afisa elimu taaluma sekondari wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro Bi Stella Mwangomale amesema kuwa mradi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya wasichana Machame upo katika hatua nzuri na kwamba mradi huo utakamalika ndani ya siku kumi na tisa.
Stella ameyasema hayo Leo Mei 29,2025 alipofika shuleni hapo Kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bweni hilo.

Amesema kutokana na kazi kufanyika kwa haraka imepelekea kufika hatua ya ukamilishaji na kwamba baada ya kukamilika mradi huo utakabidhiwa.
“Tunaamini kabisa katika siku hizi zilizobakia,zimebaki siku 19 , na kazi inavyoonekana itamalizika hata kabla ya hizo siku 19, na itamalizika salama”Amesema Stella Mwangomale.
Kwa upande wake makamu mkuu wa shule ya wasichana Machame sekondari Devartusi Swai akatoa shukrani zake kwa serikali Kwa kupeleka fedha kwa ajili ya mradi huo.
“Awali ya yote niishukuru serikali kwa ajili ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya bweni hili”Amesema Swai.