Boma Hai FM
Boma Hai FM
25 May 2025, 8:49 am

“Ni kweli Mradi huu tunategemea utazinduliwa na mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu, tunaishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kuleta mradi huu kwa kushirikiana na wananchi wa Donyomurwa “
Na Elizabeth Mafie- Siha Kilimanjaro
Ujenzi wa daraja la upinde wa mawe llilopo Kijijii cha Donyomurwa kata Donyomurwa Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro limefikia asilimia 98 kukamilika na linatarajiwa kuzinduliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru Julai 2025.
Haya yamesemwa na Diwani wa Kata hiyo Lwitte Ndossi ,alipotembea Daraja hilo kwa lengo la kukagua maendeleao ya ujenzi ambapo amesema hadi kukamika litagharimu zaidi ya milioni mia tatu.
“Ni kweli Mradi huu tunategemea utazinduliwa na mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu, tunaishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kuleta mradi huu kwa kushirikiana na wananchi wa Donyomurwa “amesema Ndosi
Ndossi,amesema mradi huo utaondoa changamoto za muda mrefu katika eneo hilo kwani wananchi wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali ikiwemo kusombwa na maji na hata wakati mwingine kufariki dunia wakati wakivuka upande wa pili kufuata huduma mbalimbali za kijamii.

Ameeleza kuwa zaidi ya wananchi elfu tatu wa vijiji vya loiwa ,Embokoi, Donyomurwa wataondokana na chanagmoto hiyo, na kwamba daraja hilo ni kuiganishi cha mawasiliano na kijijii cha Mungushi kilichopo Wilaya Hai.
Mwenyekiti wa kijijii cha Donyomurwa Meshack Laizer amesema kukamilika kwa Mradi huo kutusaidia kuondoka adha ya wanafunzi wanaosoma shule ya msingi Kwamankuu kushindwa kwenda shule hasa kipindi cha mvua hivyo kushindwa kupata masomo kwa ukamilifu.
Peter Laizer moja ya Wananchi hao wamesema kukamilika kwa mradi huo ,kutachangia ukuaji wa uchumi katika hilo,na kupunguza gharama na muda wa safari.
Mwananchi huyo akapata wasaa wa kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha kwenye mradi huo “ ameonyesha anatujali, hatuna budi ya kusema asante pia mbunge wetu wa jimbo Godwin Mollel pamoja na diwani wa kata tunawapa shukurani” Amesema Piter Laizer.