Boma Hai FM
Boma Hai FM
22 May 2025, 11:32 pm

Mkuu wa Wilaya ya Hai Hassan Bomboko amefanya mkutano na wafanyabiashara wa wilaya ya Hai baada ya wafanyabiashara hao kukiuka mikataba ya vibanda walivyokodishiwa na Halamsahauri kwa kuongeza kenop.
Na Eliya Sabai
Mkuu wa Wilaya ya Hai Mh. Hassan Bomboko amekutana na kuzungumza na wafanyabiashara waliopo ndani ya stendi ya mabasi ya Boma’ngombe katika mkutano maalum ulifanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Hai.
Mkutano huo umekuja baada ya kuibuka maswali mengi kwa wafanyabiashara waliopo ndani ya stend ya mabasi Bomang’ombe wilayani Hai baada ya tangazo lililotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Hai lakuwataka wafanyabiashara kubomoa sehemu za mbele za vibanda vyao( kenopu)walizokuwa wamejenga kinyume na mkataba waliokuwa wamekubaliana na Halmashauri ya Hai
Katika Mkutano huo wafanyabiashara walipata nafasi yakueleza changamoto zao nakusikilizwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai kabla ya mkuu wa Wilaya kujibu changamoto zao,baadhi ya wafanyabiashara wa ndani ya stendi ya Mabasi wameeleza sababu zilizowafanya kuongeza sehemu ya mbele ya biashara zao wakidai kuwa nikutokana na ongezeko la ukubwa wa biashara pamoja na eneo wanalofanyia biashara, vilevile wameiomba serikali ya Wilaya kuweka utaratibu mzuri wa gari binafsi kuingia ndani ya soko hilo ili kutoa fursa kwa wateja wao kuingia na kununua bidhaa zao bila kuhofia kupigwa fine na mzabuni wa stendi hiyo ya Bomang’ombe.

Baada yakusikiliza kero na changamoto za wafanyabiashara Mkuu wa wilaya ya Hai Hassan Bomboko amewaambia wafanyabiashara hao kuwa Serikali ya awamu ya sita inawajali sana wafanyabiashara na lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wanafanya kazi katika mazingira salama ili kukuza biashara zao na vipato vyao visonge mbele, lakini pia DC Bomboko amewataka wafanyabiashara kuwa na mawazo mbadala ya kuziangalia fursa zingine za maeneo ya kufanya biashara wilayani hapo.
Baada ya kumalizika kwa mkutano maalum wa wafanyabiashara wa soko la Mabasi Boma’ngombe wamesema wameridhishwa na majibu yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya na kuahidi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa katika mkutano huo pamoja na kuzingatia mikataba wanayopewa na Halmashauri ya Wilaya ya Hai.