

5 April 2025, 8:29 am
Katibu mpya CCM Hai apokelewa kwa matarajio makubwa ya mageuzi ya kisiasa
Na James Gasindi.
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Hai, tarehe 4 Aprili 2025, imeshuhudia tukio muhimu la makabidhiano rasmi ya ofisi ya Katibu wa CCM wilayani Hai.
Katika hafla hiyo, Katibu aliyemaliza muda wake, Ndg. Ally Ballo, alikabidhi rasmi majukumu kwa Katibu mpya, Ndg. Mkaruka Kura. Ndg. Ballo amehudumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu na sasa anastaafu kwa heshima kubwa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, viongozi wa chama wilayani hapa walimpongeza Ndg. Ballo kwa utumishi wake uliotukuka na kumtakia maisha marefu, yenye afya na baraka tele katika kipindi chake cha kustaafu.
Wakati huo huo, Katibu mpya Ndg. Mkaruka Kura alipokelewa kwa shangwe na matumaini makubwa, huku akiahidi kuendeleza misingi ya chama na kushirikiana kikamilifu na viongozi na wanachama katika kuimarisha maendeleo ya CCM Wilaya ya Hai.
Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Hai kinamtakia kila la heri Ndg. Mkaruka Kura katika majukumu yake mapya, na kinamkaribisha kwa moyo mkunjufu.