Pambazuko FM Radio

Jamii Kilombero yakumbushwa kujali makundi yenye uhitaji

15 March 2026, 4:39 pm

Picha ya baadhi ya watoto walioshiriki futari iliyoandaliwa na DC Kyobya (Picha na Kuruthumu Mkata)

Tumekutana na wenzetu ambao mara nyingi hawakumbukwi na hawapewi ushirikiano, tukumbushane kama jamii kuwaombea na kushirikiana nao wanapohitaji msaada.

Na Nicolatha Mpaka

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, wakili Dustan Kyobya, amewaalika na kushiriki futari na makundi maalum yenye uhitaji katika futari aliyoiandaa Ikulu Ndogo ya wilaya hiyo.

Katika futari hiyo ambayo imefanyika Machi 14,2026 imewakutanisha watoto yatima, watu wenye ulemavu pamoja na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Ifakara akisema kuwa lengo ni kuyaweka karibu makundi hayo ili wasijione wametengwa katika shughuli mbalimbali za kijamii.

Picha ya DC Kyobya(Picha na Kuruthumu Mkata)
Sauti ya DC Kyobya

Baadhi ya wawakilishi wa makundi maalum waliohudhuria futari hiyo wameeleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo, ikiwemo uhitaji wa msaada na ushirikiano kutoka kwa jamii ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendeleo.

Sauti za makundi yenye uhitaji

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya huyo, Mh. Kyobya, amewataka viongozi wa dini pamoja na wadau kutoka sekta za serikali na binafsi kuendelea kuyakumbuka makundi maalum, hususani katika kipindi hiki cha mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma ili kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili.

Sauti ya DC Kyobya