Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
9 March 2026, 7:51 pm

Picha ya Wanawake Morogoro wakiwa wameshika bango kusherehekea siki yao(Picha na Kuruthumu Mkata)
“Kuna watu watendaji wanaona mwanamke ananyang’anywa ardhi anabariki nikimsikia mtu anaangalia unyanyasaji wa namna hii ahame mkoa wangu”
Na Amina Mrisho
Watendaji wote wa serikali kuanzia ngazi ya kijiji katika mkoa wa Morogoro wametakiwa kutenda haki na kuzingatia usawa kwenye mashauri mbalimbali hasa yanayohusu wanawake na wajane.
Agizo hilo limetolewa March 8 na mkuu wa mkoa huu Adam Kigoma Malima wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Fulwe,kata ya Mikese,Halmashauri ya Morogoro yeye akiwa mgeni Rasmi.
RC MALIMA…WATENDAJI
Malima pia amewaomba wanawake kutokua wanyonge katika kutetea haki zao na za watoto wao.

Malima pia amewaomba wanawake kutokua wanyonge katika kutetea haki zao na za watoto wao.
Nae jaji mfawidhi wa mahakama ya Tanzania kanda ya Morogoro Mh. Rose Ibrahim amewataka wanawake kutumia nafasi zao vizuri ili kuionesha jamii kuwa wao ni watu muhimu.

Picha ya Mh.Rose Ibrahim Jaji Mahakama kuu kanda ya Morogoro(Picha na Kuruthumu Mkata)
Katika risala iliyosomwa na mwalimu Sharifa Bosi wa shule ya msingi Fulwe,serikali imeombwa kuendelea kupiga vita mila na Desturi zilizopitwa na wakati.
Siku ya wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo March 8 ikiwa na kauli mbiu mbalimbali na kauli mbiu ya siku hiyo kwa mwaka huu ni “Haki sawa kwa wanawake na wasichana: msingi jumuishi kufikia Dira ya 2050.”