Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
21 October 2025, 6:20 pm

“Nimeona fursa ya mimi kulipa fadhila kwa jamii iliyonikuza kwa mfumo wa Siasa kuhakikisha kunakuwa na maadili ya watoto wetu kwa mustakabali wa Taifa letu”
Na Katalina Liombechi
Mgombea udiwani Kata ya Viwanjasitini kupitia National League for Democracy NLD Abdallah Mng’ombe ametaja vipaumbele vyake na nia yake ya kuwatumikia wananchi wa kata hiyo endapo apata ridhaa kutoka kwa wananchi itakapofika Oktoba 29,2025
Akizungumza hii leo Mgombea huyo amesema Miongoni mwa vipaumbele vyake kuwa ni pamoja na kuhakikkisha jamii ya eneo hilo inakuwa na mwenendo mzuri wa Maadili,vijana wanajengewa misingi ya kujiajiri ili wawe uchumi wa kizalendo utakaowafanya walipe kodi kwa hiyari.
Aidha amesema katika uwakilishi wake matamanio yake ni kuona jamii inanufaika na rasilimali zilizopo,huduma za afya pamoja na kuhakikisha kunakuwa na maeneo ya maziko katika baadhi ya maeneo yenye changamoto hiyo.