Pambazuko FM Radio

Wanne waponzwa na meno ya tembo Moro

18 October 2025, 9:06 pm

Picha ya meno ya Tembo yaliyokamatwa na jeshi la Polisi(Picha na Kuruthumu Mkata)

Jitihada za jeshi la polisi zimeendelea kuzaa matunda ya kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kwa kutumia njia za kuwashirikisha wananchi

Na Katalina Liombechi

Katika kuendeleza mikakati ya Usalama Mkoani Morogoro Jeshi la Polisi Mkoani humo kupitia Oparesheni zake kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kuwakama watu sita kwa tuhuma mbalimbali.

Kwa mujibu wa Jeshi hilo wanne kati ya hao walikamatwa na meno ya tembo ambao wametajwa kwa majina.

Kamanda wa Jeshi hilo Alex Mkama akizungumza na waandishi wa Habari hii leo Oktoba 18,2025 akiwa Ifakara Wilayani Kilombero amesema Operesheni hiyo ni ya kuanzia Oktoba 1,2025 katika Wilaya za Kilombero,Mvomero na Morogoro.

Picha ya Kamanda Mkama(Picha na Kuruthumu Mkata)

Jeshi la Polisi limeendelea kuomba ushirikiano kutoka kwa Wananchi kuripoti taarifa za uhalifu na wahalifu.