Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
16 October 2025, 6:52 pm

“Tuone ya kwamba mtoto wa mwenzako ni wako unaweza kumpa msaada”
Na Nicolatha Mpaka
Uongozi wa Shirika la Enlighten Development Organiozation EDO linalopatikana Ifakara Morogoro umempongeza Bw. Zeno Kakweche kwa kutimiza ahadi yake ya kumnunulia mashine ya kushonea binti Maria Paula, mhitimu wa kituo cha EDO.
Bw. Zeno alitoa ahadi hiyo tarehe 14 Oktoba mwaka huu, wakati wa mahafali ya kituo hicho, na leo ametekeleza kwa vitendo kwa kumkabidhi rasmi cherehani hiyo mbele ya viongozi wa shirika.

Mkurugenzi Mwenza wa EDO, Bi. Josephine Saidi, amesema wametambua moyo wa upendo wa Bw. Zeno na kupongeza hatua hiyo iliyotolewa mapema kuliko walivyotarajia.
Kwa upande wake, mlezi wa kituo cha St. Laurenti, Bi. Rose Laurenti Njige, ameishukuru EDO na mfadhili huyo kwa kusaidia kutimiza ndoto za binti huyo anayelelewa kituoni hapo.
Maria Paula mwenyewe ameonyesha furaha na kutoa wito kwa vijana wenzake kutokata tamaa, bali kupambana ili kufikia ndoto zao.