Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
11 October 2025, 10:38 am

TARURA imekuwa na dhima ya kupanga,kusanifu,kujenga na kufanya matengenezo ya mtandao wa barabara za wilaya kwa ajili ya matokeo endelevu ya kijamii na kiuchumi
Na Katalina Liombechi
Wakala wa Barabara mijini na Vijijini TARURA Mkoa wa Morogoro wameketi Ifakara kwa siku mbili kuja na Mikakati wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara zenye changamoto.
Kwa mujibu wa Meneja wakala hiyo Mkoa huo Emmanuel Ndyamukama amesema kikao hicho kimeambatana na ziara ya kutembelea barabara ya Namwawala katika Halmashauri ya Mlimba ili kuona kama wanaweza kuanza nayo katika utekelezaji wa ukarabati.

Akifungua kikao hicho Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kilombero Abraham Mwaikwila kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Wakili Dunstan Kyobya amesema miundombinu ya Barabara ni muhimu katika kuvutia fursa za uwekezaji na maendeleo mengine.

Naye Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilombero Mhandisi sadiki karume amesema kuwa kikao hicho kinalenga kujadili changamoto na mikakati ya kuhakikisha barabara zinapitika misimu yote ya mwaka.
