Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
11 October 2025, 10:06 am

Benki ya CRDB ina asilimia 1 kwa ajili ya jamii kuchangia maendeleo ya serikali
Na Katalina Liombechi
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja Benki ya CRDB imewajibika kwa kukabidhi Viti na Meza 50 katika shule ya Sekondari Mahutanga Halmashauri ya Mji wa Ifakara ikiwa ni sehemu kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Kwa mujibu wa Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kati Chabu Mishwaro amesema CRDB imekuwa na utaratibu wa kutoa asilimia moja kurejesha kwa jamii kuchangia maendeleo kwa kugusa sekta mbalimbali kupitia programu ya “keti jifunze” kwa lengo la kuhakikisha mwanafunzi anapata utulivu anapojifunza darasani kama walilivyofanya katika shule hiyo.

Mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Oktoba 08,2025 Mkuu wa Wilaya ya Kilombero wakili Dunstan Kyobya ameishukuru benki hiyo kwa kuunga mkono jitihada za serikali licha ya kuwa bado kuna upungufu wa viti na meza zingine 184.

Sauti ya DC Kyobya
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema awali walikuwa wanapata changamoto ya wengine kukaa chini na kukaa wawili katika kiti kimoja hivyo kwa kupata viti na meza imepunguza adha hiyo.
