Pambazuko FM Radio

Bil 1.6 kunufaisha kiuchumi vijana wa kike

6 October 2025, 7:12 pm

Picha ya Vijana wanufaika mradi himilivu wa mifumo ya chakula(picha na Kuruthumu Mkata)

Katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara, utekelezaji wa mradi huu unafanyika katika kata za Katindiuka, Signali, Kiberege, na Kisawasawa, ambako vijana wanalengwa moja kwa moja kwa ajili ya kupata mafunzo, mitaji, na vifaa vya kuendeleza kilimo cha kisasa chenye tija

Na Katalina Liombechi

Katika kuhakikisha vijana wanainuka kiuchumi kupitia kilimo zaidi ya shilingi bilioni 1.6 zimetolewa kwa ajili ya kuwawezesha vijana wa kati ya umri wa miaka 18 hadi 35, kupitiamradi wa mifumo himilivu ya chakula na uwezeshaji wa biasharaya mazao yampunga na mboga mboga.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Mradi huo Dkt.Hamisi Tindwa akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo wa RUFORUM Ifakara hii leo Oktoba 6,2025 katika Ukumbi wa Mazingira amesema unalenga kuwainua kiuchumi asilimia 70 ya vijana hasa wa kike katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Morogoro, ukiwa unatekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Morogoro Mjini, Morogoro Vijijini, pamoja na Mpimbwe Mkoani Katavi.

Picha ya Dkt.Hamisi Tindwa Mratibu wa Mradi(Picha na Kuruthumu Mkata)
Sauti ya Dkt.Hamisi Tindwa Mratibu wa Mradi

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya amesema mradi huo utaleta tija kwa vikundi 18 katika Halmashauri ya mji wa Ifakara na kwamba kufanya vijana kujitegemea kiuchumi na kuwa na uwezo wa kuwaajiri wengine.

Picha ya Mh.Dunstan Kyobya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero(Picha na Kuruthumu Mkata)
Sauti ya DC Kyobya

Mkuu wa Idara ya Kilimo Halmashauri ya Mji wa Ifakara Dkt Yuda Mgeni amesema mradi huo umekuja kuleta matumaini kwa vijana kuongeza ujuzi,ubunifu na hivyo kupata tija ya uzalishaji na kujitegemea kiuchumi.

Picha ya Dkt.Yuda Mgeni Mkuu wa Idara ya Kilimo Ifakara(Picha na Kuruthumu Mkata)

Kwa upande wake Afisa maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara ameendelea kuwahimiza vijana kujiunga kwenye vikundi ili kunufaika zaidi na fursa za namna hiyo.

Picha ya Bi Florence Mwambene Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii(Picha na Kuruthumu Mkata)
Sauti ya Bi.Florence Mwambene

Wanufaika na Mradi huo kutoka Ifakara wameeleza matarajio yao.

Sauti ya Wanufaika wa Mradi

Kupitia mradi huu, vijana wanatarajiwa kupata ujuzi na nyenzo muhimu za kuendesha kilimo kama biashara, ikiwa ni sehemu ya juhudi za taifa kubadili mtazamo kuhusu kilimo na kuwa chachu ya ajira na maendeleo ya kiuchumi unatekelezwa kwa ushirikiano Vyuo vikuu vya Sokoine,Nelson Mandela,chuo kikuu cha Dar es salaam na Master Card Foundation.