Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
3 October 2025, 12:21 pm

Wazazi waomba msaada wa kifedha kiasi cha Tsh.Mil 4 na laki tatu kwa ajili ya kufanikisha matibabu ya Mtoto anayetakiwa kufanyiwa upasuaji kutokana na changamoto nadra aliyozaliwa nayo jinsi inayoleta mkanganyiko
Na Katalina Liombechi
Katika kitongoji cha magoha Kata ya Lumemo Halmashauri ya Mji wa Ifakara familia moja inapitia changamoto kubwa baada ya kupata Mtoto aliyezaliwa akiwa na viashiria vya jinsi yenye utata.
Hali hiyo imewapelekea wazazi hao kuomba msaada wa kifedha ili mtoto huyo aweze kupatiwa matibabu stahiki katika hospitali ya rufaa.
Kwa yeyote atakayeguswa na hili awasiliane na Baba wa Mtoto Adinani Mkangira kwa simu namba 0783269071.