Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
2 September 2025, 3:18 pm

Kwa mujibu wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi, kampeni za uchaguzi zilianza tarehe 28 Agosti, 2025 hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Bara
Na Katalina liombechi
Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMA leo kimezindua kampeni zake katika Wilaya ya Kilombero kuomba ridhaa kwa wananchi kuchagua viongozi wanaotokana na chama hicho ili wakafanye mabadiliko ya kimfumo na kuwaletea wananchi maendeleo katika Sekta mbalimbali.
Akieleza Vipaumbele vya chama hicho Mgombea mwenza wa U rais kupitia chama hicho Devotha Minja akiwa Ifakara Jimbo la Kilombero amesema kama wananchi watapiga kura za kutosha kuchagua Madiwani,Wabunge na Rais kutoka CHAUMA sera yao imejielekeza katika kushughulikia na kufanya maboresho katika suala la ajira kwa vijana,Miundombinu ya barabara,elimu,afya,tija kwenye kilimo na kuboresha hali ya maisha ya watu.
Aidha ametumia hadhara iliyojitokeza katika Mkutano huo ambao umefanyika leo Septemba 2,2025 katika mtaa wa Miembeni kata ya Ifakara kumwombea kura Mgombea nafasi ya Ubunge kupitia chama hicho Magreth Lipindi.

Magreth Lipindi Mgombea Ubunge Jimbo la Kilombero kwa tiketi ya CHAUMA amesema yupo tayari kuwawakilisha wananchi wa Kilombero kutokana na kuzifahamu vyema changamoto za wananchi.

Uchaguzi Mkuu wa kuwapata Madiwani,wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utafanyika Oktoba 29,2025 na kauli mbiu inasema “Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura”