Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
24 July 2025, 8:14 pm

Licha ya mafanikio ya huduma ya mawasiliano kumekuwa na upotoshaji ambao unaendelea hivyo TCRA wamekuwa na kampeni mbalimbali kudhibiti huduma ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau
Na Katalina Liombechi
Katika kukabiliana na kudhibiti upotoshaji na uenezaji wa taarifa za uongo mtandaoni Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imekuja na Kampeni ijulikanayo kama “futa delete kabisa” kuhakikisha huduma za mawasiliano zinaendelea kubaki salama kwa watumiaji.
Haya yanakuja wakati huu ambapo maendeleo ya huduma ya mawasiliano imekua kwa kiwango kikubwa na kuongezeka kwa matumizi ya intaneti hali inayopelekea changamoto za namna hiyo kutokea.
Mhandisi wa Mamlaka hiyo Kanda ya Kati Kulwa Alex Luzalia akizungumza kupitia kipindi cha Jioni leo Pambazuko FM Radio amesema kupitia kampeni ya “Futa delete kabisa” inakusudia na kuwataka watumiaji wa huduma ya mawasiliano kujiepusha kueneza na kusambaza taarifa pasi kujiridhisha zinazolenga kuchafua na kushusha utu wa mtu kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Akisisitiza juu ya lengo la kampeni hiyo Afisa TEHAMA Mwandamizi TCRA Kanda ya kati Elisha Gama ametoa wito kwa jamii kujiridhisha na taarifa husika,kujiepusha na mijadala kwa taarifa isiyo ya uhakika pamoja na kubaini taarifa za uzushi kwa kuangalia takwimu zisizo sahihi,kutumia teknolojia saidizi ya “Reverse image searching” kubaini uhalisia wa picha na video zilizotengenezwa na akili mnemba.
