Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
18 July 2025, 2:17 pm

“Kwa anayetaka kutia nia ya Ubunge nafasi iko wazi hatuna shaka na mtu yeyote anayetaka kutia nia kupitia chama chetu“
Na Kuruthumu Mkata
Chama cha ACT-Wazalendo wilayani Ulanga kimetangaza kuanza rasmi mchakato wa uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa uchaguzi ujao.
Akizungumza na Redio Pambazuko FM kwa njia ya simu leo, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo wilaya ya Ulanga Ally Omary Matwiku amesema zoezi hilo litaanza Julai 25 hadi Agosti 10, 2025.
Ameeleza kuwa chama kinakaribisha wanachama wote wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu kwa nafasi za ubunge na udiwani, akisisitiza umuhimu wa ushiriki mpana wa wanachama katika mchakato huo wa kidemokrasia.