Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
12 July 2025, 8:02 am

Kampuni ya Sun king licha ya kujihusisha na masuala ya nishati mbadala imekuwa ikitengeneza ajira kwa vijana kama njia ya kuiunga mkono serikali kukabiliana na changamoto ya ajira hapa Nchini
Na Katalina Liombechi
Kampuni ya Sun King, inayojishughulisha na huduma za nishati mbadala, inatarajia kuajiri zaidi ya vijana 300 katika kipindi cha miezi sita ijayo, kama mawakala wa kutoa huduma zake katika maeneo mbalimbali ya Bonde la Kilombero.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Biashara wa Kanda ya Pwani, Bwana Mpoki Mwakisimba, pamoja naye Diana Kajagi Meneja wa Sun King store Tanzania wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa duka jipya la kampuni hiyo mjini Ifakara.

Akizungumza mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, ameipongeza Sun King kwa hatua hiyo akisema ni ishara ya kuunga mkono jitihada za serikali katika kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana.
Wakili Kyobya pia amewakaribisha wawekezaji wengine kuja kuwekeza Kilombero, akibainisha kuwa wilaya hiyo ina fursa nyingi za biashara, kilimo na uhifadhi wa mazingira.

Baadhi ya Mawakala wamesema kwa sasa watapata urahisi wa kuwahudumia wateja kwa wakati kutokana na uwepo wa duka hilo hukuwakieleza wanavyonufaika kwa ajira hiyo kutoka Sun king.