Pambazuko FM Radio

TAKUKURU yaonya rushwa mchakato wa Uchaguzi

2 July 2025, 7:20 pm

Picha ya Jengo la Ofisi ya TAKUKURU KILOMBERO(Picha na Kilombero)

Kama taasisi tunafuatilia vitendo vyote vinavyokatazwa na sheria zetu na zile za uchaguzi

Na Katalina Liombechi

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Wilaya ya Kilombero imesema inaendelea kufuatilia vitendo vyote ambavyo vimekatazwa na Sheria za Taasisi hiyo pamoja na sheria za Uchaguzi.

Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Wilaya hiyo Agustino Mtaki ameiambia Pambazuko FM kwamba wamekuwa wakitumia njia mbalimbali ya kutoa elimu kwa wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi,wajumbe na wananchi kwa ujumla kutokubali kushawishiwa na rushwa wala hongo hasa wakati huu kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 kwani amesema rushwa ni adui wa haki na kwamba yeyote atakayekuwa na taarifa ya vitendo vya rushwa atoe taarifa kwa kupiga simu bure kupitia namba 113.

Haya yanakuja wakati  huu Mchakato wa Uchukuaji wa fomu ukiendelea ndani ya chama cha mapinduzi na hata kwa vyama vingine ambavyo bado havijaanza mchakato huo.

Picha ya Agustino Mtaki Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Kilombero(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Agustino Mtaki Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Kilombero

Kwa upande wa Chama cha Mapinduzi kupitia kwa katibu wake Gervas Ndaki amesema mchakato wa uchukuaji wa fomu ndani ya chama tayari wametoa  taratibu na miongozo kutokukutana na makundi ya watu hivyo atakayekwenda kinyume achukuliwe hatua inavyostahili.

Sauti ya Gervas Ndaki Katibu CCM Kilombero

Chama cha mapinduzi kilifungua dirisha la uchukuaji wa fomu na kurudisha kuanzia june 28 zoezi ambalo limetamatika hii leo July 2 saa kumi kamili jioni.