Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
29 June 2025, 6:28 pm

Kuna miiko ambayo imetajwa na chama kwa wanachama kutotumia midundiko,ngoma,tarumbeta anatakiwa mwanachama kwenda kuchukua fomu na kurudisha yeyote atakayevunja kanuni atachukuliwa hatua
Na Katalina Liombechi
Ikiwa mchakato wa Uchukuaji wa Fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge na Udiwani ndani ya Chama cha Mapinduzi,Katika Wilaya ya Kilombero Katibu wa Chama hicho Gervas Ndaki amewasisitiza wanachama kufuata maelekezo ya Chama kujiepusha kuvunja utaratibu.
Ndaki ameyasema hayo wakati akifanyiwa mahojiano na Pambazuko FM Ofisini kwake wakati Wanachama mbalimbali wakiendelea kujitokeza kuchukua fomu za ubunge Majimbo Mawili ya Mlimba na Kilombero pamoja na nafasi ya viti Maalumu ubunge na udiwani ambapo kwa utaratibu zinatolewa katika Ofisi za Wilaya.
Wakati huu zoezi hilo kikiendelea Katibu huyo amewataka wanachama wote wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu huku akionya kutotoka nje ya maelekezo ya chama kama kufanya shamrashamra wanapokwenda kuchukua fomu licha ya kwamba Mpaka sasa hakuna aliyefanya hivyo,sambamba na kuwaeleza wanaochukua fomu na wanachama wengine kujiepusha na viashiria na rushwa kwani Mamlaka zinazohusika zinaweza kuwachukulia hatua watakapobainika.
Aidha amesema katika chama cha mapinduzi Ukabila na Udini havina nafasi na kwamba yeyote ana fursa sawa akiwa ndani ya Tanzania.

Zoezi la kuchukua fomu na kurudisha ndani ya Chama cha Mapinduzi limeanza Juni 28,2025 na linakwenda mpaka July 2,2025.