Pambazuko FM Radio

Tabia ya wizi yaibuka Mtaa wa Miembeni

11 June 2025, 6:49 pm

Picha ya Deogratius Mwisongo Mwenyekiti Mtaa wa Miembeni(Picha na Katalina Liombechi)

Ili kukabiliana na vitendo vya wizi kunahitaji ushirikiano wa jamii nzima,uongozi wa mtaa, na hata vyombo vya usalama

Na Katalina Liombechi

Katika Mtaa wa Miembeni Kata na Halmashauri ya Mji wa Ifakara imetajwa kuibuka kwa tabia ya Wizi Mdogo mdogo hali inayorudisha nyuma maendeleo na kuibua malalamiko kwa watu.

Mwenyekiti wa Mtaa huo Deogratius Mwisongo akizungumza hivi karibuni na pambazuko FM nyumbani kwake amesema hilo huenda likachochewa na baadhi ya tabia ya vijana kujihusisha na uvutaji wa bangi na kushinda vijiweni pasi kufanya kazi hivyo kujikuta wakiingiwa na tama ya kuiba mali za watu huku akitumia fursa hiyo kuwataka vijana kuacha kujihusisha na vitendo vya namna hiyo badala yake wafanye kazi halali za kujiingizia kipato.

Hata hivyo pambazuko FM ilipohoji kama wangeweza kutumia njia ya ulinzi shirikishi kukabiliana na hali hiyo mwenyekiti huyo amesema waliwahi kutumia njia hiyo na ilisaidia pakubwa lakini iliishia njiani kutokana na baadhi ya watu kuwakatisha tamaa waliojitolea na kwamba watajipanga upya kupitia mikutano kuona namna ya kukabiliana na Wizi na tabia zingine ovu.

Picha ya Deogratius Mwisongo Mwenyekiti wa Miembeni(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Deogratius Mwisongo Mwenyekiti wa Miembeni