Pambazuko FM Radio

CAG aibua hoja za kisera Mlimba

11 June 2025, 6:34 pm

Picha ya baadhi ya madiwani Mlimba katika baraza la CAG(Picha na Kuruthumu Mkata)

Mapendekezo ya hoja hizo ni kuendelea kuomba watumishi wa sekta mbalimbali na kufanya ufuatiliaji wa namna ya kupunguza changamoto za miundombinu ya elimu na afya

Na Katalina Liombechi/Kuruthumu Mkata

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Adam Malima amesema hoja nyingi katika ripoti ya Mkaguzi wa hesabu za Serikali katika Halmashauri ya Mlimba Wilaya ya Kilombero ni za Kisera hoja ambazo utekelezaji wake haihusishi Halmashauri moja kwa moja.

Haya yamekuja katika Kikao cha Baraza la kujadili hoja za Mkaguzi wa Serikali kilichofanyika June 10,2025 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo Ifakara Mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambapo amezitaja baadhi ya hoja hizo ni Upungufu wa watumishi wa afya,Elimu na changamoto ya miundombinu.

sauti ya Mh.Adam Malima RC Morogoro

Hata hivyo Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Christina Guveti amesema tayari wameshaanza na wanaendelea ujenzi wa vituo vya Afya na zahanati ambapo zingine zinakaribia kukamilika na kwamba zitaanza kutoa huduma muda mfupi ujao.

Sauti ya Dkt Christina Guveti Mganga Mkuu

Mkaguzi Mkuu wa nje Mkoa wa Morogoro Baraka Mfugale amesema kwa jitihada ambazo zimeendelea kufanywa na Halmashauri hiyo kwa kuona umuhimu wa kazi yao kama wakaguzi kufanyia kazi maagizo wanayoyatoa hivyo wataangalia kama Wanaweza kuzifuta au vinginevyo huku Mkuu wa Mkoa akieleza kuwa serikali itaendelea kuzifanyia kazi hoja hizo na kwamba uwepo wake zinaendelea kukumbusha katika ufuatiliaji na kuzifanyia kazi.

Sauti ya Mkaguzi Mkuu wa nje Mkoa wa Morogoro Baraka Mfugale

Kwa upande wao Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mlimba Diwani Kata ya Igima Mh Innocent Mwangasa na Makamu wake Diwani wa Kata ya Uchindile Mh.Emael Ndangalas wameendelea kuishukuru serikali ya Dkt Samia kwa mambo mbalimbali ya Maendeleo na wao kujivunia hata wanapokwenda kwa wananchi.

Picha ya Innocent Mwangasa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mlimba(Picha na Kuruthumu Mkata)
Sauti za Madiwani Mwenyekiti na Makamu wake