Pambazuko FM Radio

RC Malima: Hoja nyingi ripoti ya CAG Ifakara za kujitakia

9 June 2025, 7:28 pm

Picha ya baadhi ya madiwani wakiwa katika baraza la CAG(Picha na Kuruthumu Mkata)

Nilikuwa napata malalamiko kuwa idara ya manunuzi ina shida

Na Katalina Liombechi/Kuruthumu Mkata

Ripoti ya Mkaguzi mkuu wa Nje Mkoa wa Morogoro imebaini mapungufu kadhaa Katika hoja 18 zilizotolewa na Mkaguzi huyo katika ripoti yake ya ukaguzi wa fedha na utawala kwa mwaka wa fedha uliopita katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara.

Kikao cha baraza Maalum cha kupitia ripoti hiyo kimefanyika June 8,2025 kilioongozwa na mwenyekiti wa Halamshauri hiyo Mh Kassim Nakapala na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa idara,Madiwani na wajumbe wa kamati ya fedha na uongozi.

Miongoni mwa hoja zilizoleta maswali na kuibua mjadala mkubwa ni pamoja na bajeti isiyo na uhalisia,matumizi yaliyozidi fedha za amana kiasi cha Sh Mil 287,ukiukwaji wa taratibu fedha za manunuzi ambapo Mgeni rasmi katika Baraza hilo maalum Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Adam Malima katika hotuba yake ameelezea masikitiko yake juu ya hoja hizo akieleza kuwa ni za kujitakia na ni ishara kwamba madiwani wameshindwa kukemea upotevu wa fedha jambo ambalo athari zake ni kusua sua kwa miradi ya maendeleo hivyo wananchi kushindwa kunufaika.

Picha ya Mh.Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (Picha na Kuruthumu Mkata)
Sauti ya RC Malima,Baraka Mfugale CAG na Nicholaus Haraba Mtunza hazina Ifakara

Aidha Mkuu wa Mkoa ameitaka menejimenti kuwa na kawaida ya kuwapeleka madiwani kupata mafunzo ya mara kwa mara ili waweze kuwa na ufuatiliaji mzuri wa fedha na miradi.

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mh.Kassim Nakapala wamesema wamepokea na kuzifanyia kazi hoja hizo huku wakieleza kuwa changamoto katika idara ya manunuzi zimekuwa za kujirudia hivyo kukwamisha mambo mengi ambapo pamoja na mabo mengine wamekiri kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhoji kwa kina wametumia fursa hiyo kuomba kupatiwa mafunzo hali itakayosaidia kupunguza hoja za namna hiyo.

Picha ya baadhi ya madiwani wakiwa katika Baraza la CAG Ifakara(Picha na Kuruthumu Mkata)
Sauti ya baadhi ya madiwani wakiwa katika Baraza la CAG Ifakara

Awali akitoa elimu ya Maadili Bi Jacquilline Msumba Afisa maadili Mkoa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma Kanda ya Mashariki amesema ni muhimu kufuata misingi ya maadili kwa kufanya kazi kwa uaminifu na kujali ili kuleta haki na huduma saawa kwa wananchi.

Sauti ya Bi Jacquilline Msumba Afisa maadili Mkoa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma Kanda ya Mashariki