Pambazuko FM Radio

Kilombero haitamani dosari zoezi la uhakiki taarifa za mpiga kura

16 May 2025, 8:30 pm

Na Katalina Liombechi

Picha ya Zuhura Mussa na Lucian Chigangwe wakihakiki taarifa zao kituo cha chekechea Kata ya Kibaoni(Picha na Katalina Liombechi)

Zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura awali lilifanyika mwezi Machi na kwa mwezi huu mei kuanzia leo tarehe 16 hadi 22 ni katika kuhakiki taarifa hizo na wengine kujiandikisha kwa wale walioshindwa kujiandikisha mwezi machi mwaka huu

Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kuhakiki na kujiandikisha katika daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba Mwaka huu.

Zoezi hilo la siku saba limeanza rasmi leo, Mei 16, 2025, na linahusisha kuhakiki taarifa za wapiga kura waliopo tayari kwenye daftari pamoja na kuwapa fursa wale ambao hawajawahi kujiandikisha kufanya hivyo kwa mara ya kwanza.

Akizungumza Afisa huyo Daniel Msigwa amesema zoezi hili ikiwa ni awamu ya pili litafanyika katika vituo 20 pekee ambapo ni kituo kimoja kwa kila kata isipokuwa kata ya Mwaya kuna vituo 2 kutokana na jiografia ya eneo hilo.

Sauti ya Daniel Msigwa Afisa uchaguzi Jimbo la Kilombero
Picha ya Daniel Msigwa Afisa uchaguzi Jimbo la Kilombero(Picha na Katalina Liombechi)

Aidha, aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kuhakikisha wanawahamasisha wanachama wao na wananchi kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili liweze kufanikiwa kama ilivyokusudiwa.

Sauti ya Daniel Msigwa Afisa uchaguzi Kilombero

Kwa upande wao, wawakilishi wa vyama vya siasa  akiwemo Mwakilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa nafasi ya mwenyekiti Wilaya ya Kilombero Remigi Maginga naye mwakilishi wa Chama cha mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya Katibu Wilaya ya Kilombero Gervas Ndaki wameelezea Mitazamo yao na namna wanavyohamasisha wanachama wao kushiriki zoezi hilo.

Sauti za Remigi maginga na Gervas Ndaki Wawakilishi wa vyama vya siasa

Hata hivyo baadhi ya Wananchi waliojitokeza kuhakiki taarifa zao katika Kituo cha Chekechea Kata ya Kibaoni walikuwa na haya ya kusema.

Picha ya baadhi ya wananchi waliofika kuhakiki na kujiandikisha kituo cha Chekechea Kibaoni(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti za wananchi waliofika kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Kituo cha chekechea

Kwa upande wake Afisa mwandikishaji Msaidizi ngazi ya Kata ya Kibaoni Robert Mbega amesema zoezi hilo tangu lilipoanza mapema leo asubuhi linakwenda vizuri na mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa huku akiomba kuongezewa kituo kingine kutokana na Jiografia ya eneo hilo kwamba inaweza kupelekea wengine wakapitwa na zoezi hilo muhimu.

Picha ya Robert Mbega Afisa mwandikishaji msaidizi kata ya Kibaoni(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Robert Mbega afisa mwandikishaji Msaidizi kata ya Kibaoni