Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
22 February 2025, 7:43 pm

“Sisi Watu wenye ulemavu kwa muda mrefu hatujakumbukwa ila tunashukuru kwa huyu mdau Issa Vitus Lipagila kwa kutushika mkono sasa tutafanikisha shughuli zetu kwa kuepuka kupata ajali zisizokuwa za lazima[“Walemavu wasioona
Na Elias Maganga
Walemavu wasioona Kilombero wamepatiwa msaada wa fimbo nyeupe 50uliogharimu Tsh,1,500,000/=kutoka kwa mdau Issa Vitus Lipagila ambazo zitawawezesha kutembea ili waweze kufanikisha shughuli zao kwa kuepuka kupata ajali zisizokuwa za lazima.
Msaada huo umetolewa baada ya uongozi wa chama cha wasioona Wilaya ya Kilombero kupitia katibu wake Bwana Donath Tulutulu kumwandikia barua ya maombi ya fimbo nyeupe 50 February 3 mwaka huu ambapo pia mbali na kumshukuru wamemuomba awasidie wapate ofisi ya chama chao,huku Mwenyekiti wa cha cha wasioona Wilaya ya Kilombero Bwana Ismail limbega amewaomba wananchi kwa ujumla wasiuhusishe msaada huo na masuala ya kisiasa kwani msaaada huo ni upendo wa mdau huyo kwa walemavu wasioona .

Akizungumza na walemavu wasioona febr22,2025 katika shule ya msingi Ifakara wakati akiwapatia walemavu hao fimbo 50 Bwana Issa Vitus Lipagila amesema mahitaji yote waliyoyaomba ya kupata jengo la ofisi na kufanya kampeni ya kupita nyumba kwa nyumba ili kuwabaini walemavu ambao baadhi inadaiwa mpaka sassa bado wanafungiwa ndani.
Amesema kampeni ya kupita nyumba kwa nyumba ili kuwabaini walemavu ambao baadhi inadaiwa mpaka sassa bado wanafungiwa ndani inaanza mapema huku upatikanaji wa uwanja na ujenzi wa ofisi ukifanyiwa kazi mara moja

Baadhi ya walemavu waliopatiwa msaada wa fimbo nyeupe wamemshukuru mdau huyo na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuwasidia kwani walemavu wana mahitaji mengi ambayo jamii kwa ujumla inatakiwa kuwajali kwani walemavu ni watu kama walivyo wengine

Rais Dr Samia Suluh Hassana anaingia madarakani alikaa na walemavu nchi nzima jijini Dodoma na kuzungumza nao
Hiyo ni ishara ya kuonyesha upendo katika kundi hilo.