Pambazuko FM Radio

DC Kyobya ataka Udhibiti Mawakili Vishoka wanaotapeli wananchi-Kilombero

3 February 2025, 8:02 pm

Na Kuruthumu Mkata

Picha ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero akiwa na Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Kilombero katika kilele Wiki ya Sheria(Picha na Kuruthumu Mkata)

Mkuu wa wilaya ya kilombero wakili Dunstan Kyobya ameliagiza jeshi la polisi wilayani humo kuhakikisha mawakili vishoka  wanaotapeli wananchi wanakamatwa mara moja ,huku akisisitiza ushirikiano kwenye jambo hilo

Hayo amezungumza katika hafla za kilele cha wiki ya sheria yaliyofanyika leo February 3,2025 katika viwanja vya mhakama ya wilaya ambapo amesema kuwa kuna mawakili wanaosema wao ni mawakili kumbe hata vigezo hawana ikiwemo leseni na kutumia njia hiyo kuwatapeli watu

Aidha Mh.Kyobya ameliagiza jeshi la polisi wilayani kilombero kuhakikisha vishoka hao wanakamatwa mara moja,huku akimuelekeza hakimu wa Wilaya hiyo kuhakikisha wakili yoyote anakayejitokeza mbele yake ahakikishe anakuwa na leseni kwa kufanya hivyo kutaondoa utapeli kwa wananchi.

Picha ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero akizungumza kilele Wiki ya Sheria(Picha na Kuruthumu Mkata)

Kwa upande wake hakimu mfawidhi wa wilaya ya kilombero Regina Futakamba ameelezea malengo ya kauli mbiu hiyo amesema kuwa inalengo ya kukuza uchumi na pato la Taifa na kutoa hamasa kwa taasisi zinazotoa haki madai huku akisema inakumbusha kutoa haki na usawa katika jamii.

Sauti ya Hakimu Regina Futakamba
Picha ya Hakimu Regina Futakamba(Picha na Kuruthumu Mkata)

Ikumbukwe kuwa maadhimisho ya wiki ya sheria yalizinduliwa January 25 na kilele chake ikiwe leo hii February,03 huku kauli mbiu ikisema “TANZANIA YA 2050,NAFASI YA TAASISI ZINAZOSIMAMIA HAKI MADAI KATIKA KUFIKIA MALENGO MAKUU YA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO”