Pambazuko FM Radio
Wenyeviti serikali za mitaa Ifakara watakiwa kuheshimu kiapo, kutekeleza majukumu
29 November 2024, 2:51 pm
Na Katalina Liombechi
Wenyeviti wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu na kufuata miongozo ya Serikali ili kuepuka kwenda kinyume na kiapo chao katika kuwahudumia Wananchi.