Wasiasa waelezea sintofahamu baadhi ya majina ya wagombea kuenguliwa Ifakara
20 November 2024, 7:15 pm
Na Katalina Liombechi
Wakati zoezi la Kampeni likizinduliwa leo Novemba 20,2024,Katika Halmashauri ya mji wa Ifakara imeelezwa bado kumekuwa na hali ya Sintofahamu kufuatia kile kilichoelezwa kuenguliwa kwa baadhi ya majina ya Wagombea.
Wakizungumza mara baada ya Kikao cha kupitia ratiba ya Kampeni ya uchaguzi Novemba 19,2024, baadhi ya viongozi wa vyama vya Siasa Wamesema licha ya ratiba hiyo kuwa sawa lakini kuna baadhi ya wagombea majina yao yamekatwa hivyo wamemuomba Msimamizi wa Uchaguzi kuchukua hatua za haraka ili kuondoa malalamiko hayo hatimaye wagombea wote waweze kushiriki.
Akijibia hilo Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Christopher Msimbe amesema kwenye uchaguzi kuna michakato mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mapingamizi na Rufani ambapo kuna baadhi ya watu mapingamizi yao yalikuwa halali na wamerejeshwa kuendelea na Mchakato wa Uchaguzi na wengine waliondolewa kutokana na kukosa uhalali huku katika hatua ya Rufani wengine walishinda rufani zao na wengine wameshindwa rufani hizo.
Sauti ya Afisa Uchaguzi Halmashauri ya Mji wa Ifakara Christopher Msimbe 1
Akizungumzia Kuhusu Ratiba ya kampeni Msimbe amesisitiza kampeni za kistaarabu pasi kubadili ratiba kiholela huku akisisitiza amani na utulivu.