Kikokotoo bado fumbo kwa watumishi wastaafu
3 May 2024, 12:27 am
Bango la shirika la Posta katika maandamano ya Mei Mosi – Picha na Isidory Matandula
Mishahara duni, miundo mbinu mibovu, mikataba mibovu ya ajira, kuchelewa posho za uhamisho na kikokotoo cha wastaafu ni msalaba unaowaelemea watumishi .
Na: Isidory Matandula
Imeelezwa kuwa kikokotoo cha mafao ya kustaafu, kimegeuka kuwa kero badala ya faraja kwa wastaafu.
Hayo yameelezwa jana katika risara ya jumuiya ya wafanyakazi mkoa wa Morogoro iliyosomwa jana na katibu wa chama hicho bwana Nicholaus Ngowi
Katibu wa TUCTA akisoma Risara mbele mkuu wa mkoa RC Malima – Picha na Isidory Matandula
Sauti Katibu wa TUCTA – Morogoro
Paambazuko fm imepata nafasi ya kuongea na baadhi ya wafanyakazi kupata maoni yao; Mwalimu Marietha Njonjo na Mchungaji Jumanne Kisweka wamesema suala la kikokotoo ni changamoto kwa wastaafu hali inayosababisha baadhii ya kupoteza aaisha, hivyo wameiomba serikali ifanye marekebisho ya haraka ili waweze kupata stahiki zao baada ya kustaafu.
sauti za wafanya kazi
Naye mmoja wa viongozi wa mkoa wa chama cha wafanya kazi ameongea na Pambazuko fm kwa njia ya simu na kwa sharti la kutotaja jina lake ameeleza madhara ya kikokotoo cha sasa ni kutokana na asili kuwa kubwa ikilinganishwa na zamani ambapo gawio lilikuwa dogo – 1/540 na sasa ni 1/580.
sauti ya kiongozi wa TUCTA
Pambazuko imefika ofisi za PSSSF (Mfuko wa hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma) halmashauuri ya mji wa Ifakara ili kupata undani wa suala Kikokotoo baada ya kuwa moja ya changamoto kubwa zilizotajwa katika risara ya wafanya kazi siku ya MEI MOSI, ambapo afisa matekelezo Emanuel Meishaa amesema , “Kikokoto ni kanuni inayotumika kukokotoa mafao ya uzeeni”.
Nembo ya shirika la Mfuko wa hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma – Picha na Isidory Matandula
Sauti ya bwana Meishaa – PSSSF
Pambazuko fm imezungumza kwa njia ya simu na chanzo cha kuaminika, kwa sharti la kutotajwa jina kimesema si wafanyakazi wote wanaolalamika juu ya kikokootoo isipokuwa ni kundi ambalo hapo mwanzo lilikuwa linapata pensheni ya asilimia 50 ya mafao, ambapo kwa sasa mstaafu anapata pensheni ya asilimia 33 tu ya mafao yake.
Chanzo cha kuaminika
Kwa upande wake mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Morogoro Kigoma Ally Malima, amesema serikali imerejesha utaratibu wa kuwapandisha vyeo wafanya kazi kila baada ya mika mitatu, kuanzia mwaka ujao wa fedha.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro akisoma hotuba ktk maadhimisho ya Mei Mosi – Picha na Isidory Matandula
sauti ya mgeni rasmi – RC Malima
Maadhimisho ya Mei Mosi mkoa wa Morogoro yamefanyika mjini Ifakara, halmashauri ya mji wa Ifakara, katika viwanja vya CCM Tangani, ambapo kauli mbiu inasema, ‘’ “Nyogngeza ya Mishahara ni Msingi wa maafao bora na kinga dhidi ya hali ngumu ya maisha”.