Wafanyakazi Morogoro walia kwa kutopandishwa madaraja
1 May 2024, 12:11 am
Wajumbe wa halmashauri za mkoa wa MIorogooro wameketi kikao cha mwisho mjini Ifakara, kupanga na kuweka sawabajeti kuelekea maadhimisho ya Mei Mosi 2024
Na: Isidory Matanddula
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani katika mkoa wa Morogoro yatafanyika katika halmashauri ya mji wa Ifakara, uwanja wa kwa Tangani (uwanja wa Taifa) ambapo mgeni rasmi atakuwa kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Kigoma Adam Malima
Akizungumza na Pambazuko fm, nje ya ukumbi wa mkutano, mwenyekiti wa Chama Cha wafanyakazi mkoa wa Morogoro Mwl. JUMANNE NYAKIRANG’ANI amesema miongoni mwa madai ya wafanyakazi mkoani Morogoro ni pamoja na; suala la mishahara, Likizo, uhamisho wa watumishi, Pesa za kufundishia na Pesa za mazingira magumu.
Pichani ni kushoto katibu na kulia ni Mwenyekiti – Picha na Isidory Matandula
Sauti ya Mwenyekiti -Mwl Nyakirang’ani
Kwa upande wao wajumbe wa mkutano huo; bwana Ramadhani Ng’atang’ata, bi. Mwanaharusi Kitema na Mwalimu Fesi Peter, wameiambia Pambazuko fm kuwa serikali iangalie suala la Malimbikizo ya mishahara, Pesa za Likizo, Kikotoo na tabia ya baadhi sekta binafsi kuwachisha wafanyakazi kiholela bila kufuata sheria.
Sauti za wajumbe
Naye katibu wa chama cha wafanyakazi mkoa wa Morogoro bwana Nicolaus Ngowi, ametoa wito kwa watumishi wa mkoa wa Morogoro kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo ili waweze kutetea kauli mbiu inayosema “Nyogngeza ya Mishahara ni Msingi wa mafao bora na kinga dhidi ya hali ngumu ya maisha”.
Sauti ya Katibu Nicolas Ngowi