Pambazuko FM Radio

TAWA: Pori la akiba Kilombero lazima lilindwe kwa nguvu zote

20 February 2024, 11:51 am

Pori la akiba la Kilombero ni chanzo kikubwa cha maji katika mradi mkubwa wa kufua umeme katika Bwawa la Mwalimu Nyerere hivyo kuna kila sababu ya kulilinda ili mradi huo wa kimkakati uweze kukamilika

Na Elias Maganga

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania { TAWA},Wilaya ya Kilombero imesema itaendelea kulilinda na kulitunza Pori la akiba la Kilombero,kwa njia yoyote kwa sababu  lina manufaa makubwa kwa Taifa ikiwa ni chanzo cha maji katika Bwawa la Mwalimu Nyerere.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Kamanda wa kanda ya nyanda za juu kusini{TAWA} Alphonce Mung’ong’o baada ya askari wa TAWA Wilaya ya Kilombero kukamata ng’ombe 1480 wakichunga ndani ya hifadhi ya pori hilo la akiba.

Kamanda Mung’ong’o amesema wataendelea kufanya operesheni za kuwakamata wafugaji wanoendelea kuingiza mifugo kwenye hifadhi ya pori hilo ili kuhakikisha hifadhi inakuwa salama.

Picha ya Kaimu Kamanda wa kanda ya nyanda za juu kusini{TAWA} Alphonce Mung’ong’o{Picha na Elias Maganga}

Sauti ya Kaimu Kamanda wa kanda ya nyanda za juu kusini{TAWA} Alphonce Mung’ong’o

Amesema wamekuwa wakitoa elimu tangu kuanzishwa kwa hifadhi hiyo kwa wananchi kutofanya shughuli za kibinadamu kama vile ufugaji,kilimo,uvuvi haramu na uwindaji haramu,pamoja na utolewaji wa elimu hiyo lakini kuna watu wachache ambao wamekuwa wakikaidi utii wa sheria bila shuruti na TAWA huwakamata na kuwachukulia hatua.

Sauti ya Kaimu Kamanda wa kanda ya nyanda za juu kusini{TAWA} Alphonce Mung’ong’o 2

Je wito wake kwa wananchi ni nini?Kamanda Mung’ongo huyu hapa anaeleza.

Sauti ya Kaimu Kamanda wa kanda ya nyanda za juu kusini{TAWA} Alphonce Mung’ong’o

Afisa wa uhifadhi daraja la kwanza katika Bonde la Kilombero ‘A’ Bedui Mboto amesema mifugo hiyo 1480 iliyokamatwa 394 tayari imeshalipiwa faini ya shilingi laki moja kwa kila ng’ombe huku zoezi la ulipaji wa faini likiendelea huku wafugaji  wakitakiwa kurudi   kule walikotoka.

Aidha Kamanda Mboto amesema kukamatwa kwa mifugo hiyo  imetokana na ushirikiano kati ya wahifadhi na wananchi na hiyo itasaidia maeneo ya wananchi yatakuwa salama na wananchi wa mkangawalo watalima na kuvuna bila ya kuwepo kwa changamoto ya wafugaji kulisha mazao ya wakulima.

Picha ya Afisa wa uhifadhi daraja la kwanza karika Bonde la Kilombero ‘A’ Bedui Mboto
Sauti ya Afisa wa uhifadhi daraja la kwanza katika Bonde la Kilombero ‘A’ Bedui Mboto